Inasikitisha na kushangaza saana unapoona na pengine kusoma jinsi serikali inavyojua kile kinachoimung'unya jamii na kuishia kusema TUNALIFANYIA KAZI. Na hapo hakuna kitakachoendelea. Nimesoma takwimu mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu maisha ya waTanzania na ambazo bila ubishi zinaonesha kuwa yako hatarini kuliko miaka ya nyuma na nabaki najiuliza kama WATAWALA wetu (najisikia vibaya kuwasingizia kuwa ni viongozi) wanajua kinachotakiwa kufanyika ili kuwanasua wananchi na matatizo haya. Hili toleo lililoandikwa kwa Dada Koero (bofya kulisoma) ni dhihirisho tosha kuwa hakuna aliye makini na anayeguswa na hali halisi ya kinamama huko vijijini ambao wanafariki tena kwa mambo ambayo yangeweza kuzuilika. Takwimu hizi ni mbaya saaana, lakini ni nani anayeweza kuamini kuwa hizi ni takwimu halisi? "Viongozi" wetu hawana mpango na huko watokako. Hawaendi na hawajui kama wanazopewa ndio takwimu halisi ama ni yale yale ya Rais kupewa takwimu za miaka 12 iliyopita (Bofya hapa kama hukuisoma hii). Na kama hizi takwimu si sahihi (jambo ambalo sitashangazwa nalo) kuna harakati gani wa kuwajibisha wanaozitunza na kuzishughulikia ili kuhakikisha zinakwenda na wakati?
Hakuna ubishi kuwa kinachutuumiza katia tatizo la vifo vya kinamama ni miundombinu ya kuwawezesha kufika hospitali mapema, jambo ambalo hata Waziri Mkuu katika maelezo yake bungeni alilizungumzia (mkaaaavu bila hata hisia) kama unavyoweza kutazama hapa chini
Maongezi ya Waziri Mkuu ni kati ya vitu ambavyo binafsi vimenisikitisha. Yaani anaongea kama vile imekuwa mara ya kwanza kwake kusikia kuhusu tatizo hilo la vifo vya kinama wanapokwenda kujifungua, anasimuliza kuhusu ubovu wa mawasiliano ya barabara, mambo ambayo wameshindwa kuyaendeleza japo ndio zilipaswa kuwa shughuli zao za awali walipoingia madarakani. Anaishia kusema TUNALIFANYIA KAZI. Sasa anamwambia nani? Kwani ni mara ngapi tumesikia hili na yeye hajaja na maelezo yoyote kuwa wanalifanyia kazi vipi, nani anafanya ama atafanya nini, lini, vipi na matokeo yategemewe lini? Hakuna kujiwekea malengo hapa, hakuna timeline, hakuna commitment hakuna lolote. Ni Orijino Paliamenti kama ilivyo Orijino Komedi....Hii ni aibu. Anaeleza kuhusu kuwa na Zahanati za upasuaji wakati amekiri kuwa hawana barabara za kufika ziliko hizo chache. Kwani zahanati ni nini? Majengo? Tunaonsna "shule" ngapi ambazo zimejengwa na sasa hazina walimu? Ni Waziri huyu huyu aliyezungumza kuhusu uwiano wa magari ya wabunge na matrekta kuwa Gari moja la mbunge ni sawa na matrekta 20 na kuahidi kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika matumizi ya pesa za serikali akikiri kuwa watumishi hawawapi kipaumbele wananchi na akanukuliwa akisema "katika mifumo ya bajeti, tunazo pesa zinazoweza kupunguza matatizo ya kweli ya watanzania, lakini sehemu kubwa ya fedha hizo haziendi huko na badala yake zinakwenda katika maeneo ambayokwa sehemu kubwa kabisa yanatuhusu sisi watendaji na viongozi". Habari hii niliiripoti hapa Feb 11 (Bofya hapa kuisoma). Hatuna tunaloona zaidi ya madai ya nyongeza za posho za kukaa bungeni (maana siku hizi wanajitahidi wasisinzie maana wanajua wako "Live" TBC)
Kama kuna kosa basi ni kujumuisha hawa wanawake wengi wanaofariki kutokana na uzembe na kuwafanya kama namba. HAWA SI TAKWIMU, NI MAISHA YA WATU YANAYOPOTEA KWA KUWA WATU WENGINE HAWAJATIMIZA WAJIBU WAO wa kusaidiana nao kutengeneza barabara, kujenga zahanati na kutumia rasilimali zilizopo kwa manufaa ya jamii husika na sio kuiuza na kujilimbikizia mali.
Najua uchaguzi umekaribia na wapo watakaojitahidi kuigiza kujali sasa. Lakini tumewasikia, tunakumbuka na tunajua kuwa mengi mnayosema ni yale mliyowahi kusema.
Kumbukeni kuwa tunasema haya yote ili kuzuia wengine (na pengine sisi) kuwa another NUMBER IN THE BOOKNi mtazamo tu, na labda namna nionavyo tatizo ndio tatizo
Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA
1 comment:
Leo katika yale yanayoitwa 'maswali ya papo kwa papo', kuna Mbunge wa Zanzibar alimwuliza Waziri Mkuu, Pinda kuhusu ucheleweshwaji wa kifuta jasho kwa waathirika wa ghasia (mauaji ) ya Januari 2001. Mbunge akadai mwaka wa tisa lakini wananchi hawajalipwa kifuta jasho walichoahidiwa na serikali.
Samari ya majibu ya Waziri Mkuu, '...tupe muda...tunashughulika'
Mbunge yule pengine kwa kutokuridhishwa na majibu hayo rahisi akaomba Waziri mkuu ikiwezekana basi atoe tamko kwamba kifuta jasho kile hakipo kuliko kutoa majibu yale yale kila anapouliza.
Waziri Mkuu akajibu '...tukijibu hatuwezi itakusaidia nini...tupe nafasi tulishughulikie...'
Ndivyo ilivyo. Maswali yaleyale. Majibu yaleyale. Mbwembwe zilezile. Almuradi posho zinaingia.
Post a Comment