Thursday, July 16, 2009

Kina Klothing Yafungua Duka Mtandaoni

Salaam kwa wadau wote wa blogu ya CHANGAMOTO YETU.

Kina Klothing ina furaha kuwafahamisha kuwa tumefungua duka letu mtandaoni na unaweza sasa kununua Tshirt moja kwa moja kupitia www.kinaklothing.com

Kina ni kampuni mpya ya nguo ambayo inawakilisha Bongo na Afrika kwa ujumla. Kwa utambulisho tumetoka na kollektion inayoitwa Uhuru St. kwa sababu neno uhuru linabeba sababu nzima ya sisi kuanzisha Kina.

Vilevile hii ni lebo ya mavazi ya kitaa na Uhuru ni mtaa wa kwanza katika mfululizo wa kollektion zitakazobeba majina ya mitaa mbalimbali ya Bongo na Afrika kwa ujumla.

Kama kauli mbiu yetu inavyosema “Vitu vyetu. Kivyetu” basi ndio tunavyotarajia kuendesha lebo yetu, yaani full uhuru wa kutengeneza kazi zinazotuwakilisha, kwa namna tunayoamua wenyewe.

Tshirt hizi zimesanifiwa mahsusi kwa ajili ya wabongo na marafiki zao ili kuonyesha kuwa wabongo nao tumo katika medani hii ya design; lakini si hivyo tu, ujumbe unaobebwa na nguo kina ni mchango wetu katika harakati za kujenga madaraja kati ya waafrika barani na diaspora kwa kusambaza na kusheherekea yale yanayotuunga pamoja kama waafrika.

Hata hivyo, katika kollektion hii ya kwanza tumeamua “kucheza kwetu” zaidi, tunatumai utatutunza.

Tutembelee http://www.kinaklothing.com/ na tuambie mawazo yako



Pia usisahau kujiunga nasi katika ukurasa wetu ya facebook (http://www.facebook.com/pages/Kina-Klothing/101720604819) na kutufuatia katika http://www.twitter.com/kinaklothing

Kaa mkao wa kula kwa kollektion inayofuatia, Samora avenue. Iko jikoni.
Amani.
Mkuki na Susan (Kina Klothing)

Baadhi ya kazi za Kina Clothings ni hizi hapa chini.
Kwa niaba ya wana-CHANGAMOTO wote, napenda kuwapongeza KINA CLOTHING kwa kufikia malengo haya. Naamini ujumbe utawafikia wale wote wenye kutembelea "jamvi" hili.
Shukrani pekee kwa Dada SUBI kwa kuendeleza kutugawia ujuzi na taarifa mbalimbali za kuisaidia jamii yetu.

HESHIMA KWENU NYOTE

1 comment:

Anonymous said...

Inapendeza tunaposaidiana sisi kwa sisi ili kunyanyuana kutoka kwenye hili handaki la umasikini.
Asante Mzee wa Ch kwa kukubali wito wa kuwatangaza vijana!
Appreciated!