Saturday, July 25, 2009

Ni DHAMBI, HARAMU, HATARI ama ni siasa katika hili?

Miaka nenda rudi tumekuwa tukisikia kila aina ya maelezo kuhusu ubaya wa matumizi ya Bangi. Lakini wakati huohuo kukawa na ubishi wa kama yasemwayo kuhusu Bangi yana ukweli ama ni siasa nyuma ya matumizi yake. Wapo wanaosema ni DHAMBI kuvuta bangi, wengine wanasema ina athari kubwa za kimatibabu na wapo waliosema kuwa ni kwa kuwa hakukuwa na mbinu nzuri za kuilipisha kodi, ndio maana ikawa inapingwa.
Sikuwahi kujiuliza undani wa hayo mpaka wa majuzi nilipoona tangazo la Tv la kuonesha kuwa kuhalalisha bangi California yaweza kuwa suluhisho la mapungufu ya pesa ambayo jimbo hilo linakabiliwa nayo. Lakini wapo wanaounga mkono kuhalalishwa kwa matumizi ya mmea huu wakieleza kuhusu utunzaji wa mazingira utakaotokana na majani yake ambayo yanaweza kuokoa maelfu ta miti kukatwa kutengeneza karatas.
Naishia kujiuliza kuwa kwanini sasa yaonekana kuna uwezekano wa kuhalalisha kile ambacho miaka yote tumeambiwa kuwa ni kibaya?
Natamani wataalamu wa afya (kama Dada Subi, Dk Faustine na wengine) wangesaidia kuelimisha hili kwani sasa yaonekana maduka ya dawa zitokanazo na bangi yanazidi kuongezeka kwa kasi na kuzidi kuwavutia wengi kuwa hakuna madhara katika kutumia hili na hadi kufikia jana ( July 24) yasemekana kumekuwa na maduka haya mengi kuliko migahawa kama Mc Donald, Seven Eleven na mingine mikubwa katika sehemu za jimbo a California.

4 comments:

Subi Nukta said...

Ni jana mtu mmoja ameuliza swali hili hili, juu ya habari ya athari ya banghi, hashish, ndumu, jani, marijuana nk. Nikatuma linki inayojieleza vyema kutoka kwenye tovuti ya Serikali ya Marekani.
Nikiwa najibu kuweka maelezo marefu hapa, nimeshindwa kuposti kutokana na kizuizi cha idadi ya herufi zinazoruhusiwa na blogger katika kisanduku cha maoni (5000 tu), herufi zangu yangu zilikuwa yanazidi namba 5000 hivyo naona ni vyema kuweka linki ili Muuliza swali na Msomaji wapate kurejea kwa ujuzi zaidi.
Link ni hii:
http://www.nida.nih.gov/Infofacts/marijuana.html

Mzee wa Changamoto said...

Asante saaana Da Subi kwa LINK ambayo naamini wengi wataweza kuisoma na kuelimika zaidi.
Pengine tunaweza kuanza kujiuliza kuhusu HESABU ZA KISIASA kama ambavyo nilishauliza zamani. Kwa kuwa yaonesha kuna madhara kama niliyosoma, unaamini kuwa majimbo yanayoruhusu yanajali pesa na mafanikio yao ya kisiasa kuliko uhai wa watu (kama ambavyo imekuwa kwa wanasiasa wengi?)
Yaonesha sasa kinachoangaliwa ni namna ambavyo uchumi wa jimbo utaweza kurejea kuwa pale ambapo walio madarakani wataonekana wana MIPANGO THABITI kuliko "ukweli" wa athari za namna wanavyosaka kurejesha uchumi huo.
Politricks.

Fadhy Mtanga said...

Ahsante kaka Mubelwa kwa kulileta hili.
Pia shukrani kwa da Subi kwa link hiyo. Wacha nami nikaisome.

Lakini kabla sijatoka, naweka mchango wangu.

Mi naamini bangi ina madhara makubwa kuliko hizo pesa watakazozipata. Nadhani siasi inajali zaidi maslahi ya kundi fulani kuliko ustawi wa wananchi wake.

Inafahamika wazi juu ya madhara ya bangi. Wataalamu wanasema inasababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri, inadumaza akili. Na kuchochea maamuzi mabaya.

Pia inasemwa kuwa inaharibu utengenezwaji wa manii (sperms) na hivyo kuchangia uhanithi.

Inaelezwa kwamba, bangi hiyo hiyo inasababisha kansa ya mapafu na kansa ya damu.

Kama ndivyo, serikali inaona poa tu, bora pesa ipatikane! Ni kama sigara, nayo wataweka maandishi, "ina madhara kwa afya yako" ilhali matangazo yao ya biashara yanatoa ushawishi kuwa, "haya ndiyo maisha"

Kazi ipo, wala si ndogo.

Ni hayo tu!

Born 2 Suffer said...

Mada nzuri hii Mzee wa Changamoto kitu chohchote kinadhuru mwili wa binadamu ni haramu na si cha kuruhusiwa kutumika kihalali na wakati kinatumika kiharamu na kuharibu afya za watu.