Friday, July 17, 2009

Them, I and Them....AFRICANS...Innocent Galinoma

"We must start from the simple premise that Africa’s future is up to Africans." U.S President Barack Obama
Kama kuna lililotingisha bara wiki hii ni ujio wa Rais wa Marekani barani Afrika. Imekuwa ni ziara ya kwanza ya Rais huyu kutembelea bara lake la asili. Katika hotuba yake iliyoonekana kuwa HOTUBA KWA AFRIKA, Rais Obama alikumbusha yale ambayo "yameimbwa" na wanaoitakia mema Afrika kwa miaka mingi.
Kauli kuu katika hotuba yake ni hiyo iliyonukuliwa hapo juu kuwa MUSTAKABALI WA WAAFRIKA UKO MIKONONI MWA WAAFRIKA WENYEWE na hakuna anayeweza kupinga hili. Kuna ukweli ulio "mtupu" katika hili. Lakini haya yalishaelezwa na wasanii wengi na mmoja wapo ni mwana wa nyumbani Innocent Galinoma ambaye katika wimbo huu Africans aliuliza mengi ambayo hayajajibiwa na viongozi wetu.
Mwanzo wa wimbo, Galinoma anawaeleza waAfrika baraka nzote walizonazo lakini wanashindwa kuzitumia.
Well!! Tanzania ndio tuna mengi ya kujibu kuhusu hili. Mbuga za wanyama, Ardhi yenye rutuba, Madini mengi na ya thamani, Mlima Kilimanjaro, watu, Maziwa, Bahari, Mito, Mvua na hata MISAADA mingi ambayo tungeweza kuvitumia na kuwa na uwezo wa kuwawezesha wengi kuishi maisha bora kuliko ilivyo sasa lakini UONGO NA UBADHIRIFU ULIOKUBUHU vinauia haya kutokea. Katika wimbo Africans, Galinoma amewaomba viongozi wa Afrika kuwaeleza watoto juu ya yale ambayo hawayajui lakini yanaathiri maisha yao na anawaeleza viongozi kuwa
"tell the children the truth right now,
What's going on with their economy,
Rain is falling but there's no food. Why?
Where is Justice?
Where is equality?
Why theres murder, poverty and bloody everywhere?"

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hivyo ndivyo ilivyo nashangaa tunasubili obama aje kusema

hata wewe rudi home

Unknown said...

Thanks for your visit.

Greetings from Austria.

http://monimaus-monalila.de.tl

Moni

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa habari hii. Ni kweli inashangaza kwa nini hatuwezi kufanya kitu mpaka aje mtu mwingine kutuambia au kutufanyia. Nakutakia yote mema kwako na pia familia yako.