Friday, July 10, 2009

Them, I & Them. WHAT IS LIFE........Innocent Galinoma

Hivi ulibahatika kuisoma makala ya Kaka Kaluse alipouliza "JE! MAISHA YANA MAANA GANI KWETU?" (Bofya hapa kumsoma) ama Kaka Kamala kuhusu KAZI ILIYOTULETA DUNIANI? (Bofya hapa kuisoma). Makala ambayo (kwa uelewa wangu) imeeleza namna ambavyo tunahangaika kujitafuta tulipo ndani ya sehemu tuliyopotea na matokeo yake kuishia kujipoteza zaidi? Hii inakuwa ngumu maana matokeo ya maisha ya kutokuwa ulivyo hutufanya kuwa na maisha na hata tabia zisizo zetu na matokeo yake kutolipata dhumuni halisi la maisha yetu. Tunakosa furaha, upendo, amani ya roho, na hata ubunifu wa kuendeleza kazi tufanyazo na kisha tunaishia kutegemea vitu kama Rushwa ili kutusaidia kuwa pale ambapo wenye kipaji cha kazi tuifanyayo wangekuwa bila kuhangaika kama tuhangaikavyo.
Ni katikati ya mihangaiko hii unapofikia kujiuliza HIVI MAISHA NI NINI? Msanii Innocent Galinoma akiwa na kundi lake la Les Exodus waliwahi kuuliza swali hili katika wimbo wao wa What is Life. Kati ya aliyouliza Inno ni kuwa :
Is life a dream or a test? Anaendelea kueleza mengi anayojiuliza na hatimaye kuendelea kuueleza kuwa "some they say life is the gift from God, some they say life is the dream, some they say life is the misery.......Is life a Dream, or a test or a punishment for my people?"
Kwanini wengine waote maisha na wawe walivyoota na wengine washindwe? Ni kwanini wengine kwa juhudi chache wafanikiwe kuliko wengine? Ni kweli kuwa wana akili sana ama ni MAISHA tu yamewakuta mahala wanapotakiwa kwa muda wanaotakiwa?
Nimeandika mengi kumhusu Innocent Galinoma ( kama hapa na hapa) na nyimbo zake ni kati ya nyimbo njema kabisa nimewahi kuzisikia kwa wasanii wa Reggae Africa. Kama ilivyo kwa Roots Reggae, Innocent ANAELIMISHA, ANABURUDISHA na KUTUPA UKOMBOZI HALISI TOKA UTUMWA WA KIAKILI unaoonekana kusumbua wengi na hasa nchini Tanzania.
Msikilize hapa chini katika wimbo wake What is Life?

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa
IJUMAA NJEMA

4 comments:

Christian Bwaya said...

Ujumbe mzito huu! Innocent ana tungo zinazoelimisha. Nashukuru.

Yasinta Ngonyani said...

Kweli ni ujumbe mzito na unafunza mengi. Shukrani kwa hilo. Nami nakutakia Ijumaa njema pia.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

umeongelea maisha na mafanikio, bado labda tunahitaji kuyajua hayo,

eti maisha nini? na mafanikio nini au aliyefanikiwa ni yupi?

nadhani sio mala ya kwanza kuulizana maswali haya japo yaweza kuwa mara ya kwanza kupata majibu

Simon Kitururu said...

Nimesoma hapa na kusikiliza na naendelea kufikirishwa na hoja!
Ijumaa njema Mkuu!