Tuesday, July 28, 2009

Tunachagua kwa utashi ama uhitaji?

Umeshajiuliza utamchagua nani kuwa rais katika uchaguzi ujao?
Hapa sisemi jina ama chama, namaanisha SIFA za mgombea.
Ama umeshajiuliza kuwa unataka kiongozi ajaye awe na utekelezaji wa lipi na lipi na awe na ILANI inayotekeleza vipi? Ama tunasubiri waje na UONGO WAO ndio tuanze kujipanga jinsi ya kukubaliana na uongo wao? Ama mpaka waje na pesa ndio tuangalie namna zinavyoweza kutufaa? Tunasubiri waje kutuambia matatizo yetu ilhali wao hawakai kwetu? Mpaka waje na takwimu njema zisizoeleza tulivyo na kisha kutuaminisha kuwa tunawahitaji wao badala ya kuhitaji suluhisho la matatizo yetu?
Je!! Umeshamuuliza yeyote maswali haya?
Nahisi wengi hawana majibu na hili lanipeleka kujiuliza kama
TUNACHAGUA VIONGOZI WETU KWA UTASHI AMA UHITAJI?
Tuwasikilize Morgan Heritage wanavyozungumza kuhusu wanasiasa katika wimbo wao POLITICIANS. I CALL THEM POLICHEATEANS
BLESSINGS

Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

6 comments:

Fadhy Mtanga said...

Bado wengi hatujafanya uamuzi. Bado wengi tunangoja ufike wakati tutakaoshindwa kuamua vizuri kwani tayari kanga, tshirt, kofia na vikorombwezo vingine vitakuwa mbele yetu.
Bado hatujafanya maamuzi wengi wetu.
Lakini 'mwananchi mimi' nimekwishaamua sifa za kiongozi nitakayemchagua.

Albert Kissima said...

Kweli huu ni wakati mzuri kila mmoja atafakari na atafute vigezo ambavyo atavitumia katika kumchagua kiongozi bora.Ni kweli kabisa sera watakazozitoa yaweza kuwa ni za kuchonga tu hivyo mbali na sera zao nasi twatakiwa tuwe na vigezo vyetu.


Lazima pia tuwaulize wale waliokuwa madarakani walitufanyia nini ktk kila sehemu watakayosimama kuomba kura zao.

chib said...

Kawaida Wa tz huwa hawana hulka ya kutafakari mapema, wanasubiri mpaka waongo wameshapaka mafuta yanayong'aa uongo wao na kuanza kupiga porojo ndio na wao wanaanza kuamka. Ni wakati muafaka wa kuanza kujiuliza ni nini hasa tunataka kutoka kwa kiongozi. Ahsante kwa kutuamsha

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

maswali yako yooote ni mema kwani uchague usichague lazima jamaa atachaguliwa au kujichagua tu

Yasinta Ngonyani said...

Kusema kweli hatutumii utashi ni uhitaji zaidi. Na hapo ndipo tunapozidi kudidimia.

Koero Mkundi said...

Nia ya kuwaondoa viongozi wabovu ipo kwani wananchi walio wengi wanafahamu haki zao, tumeona jinsi viongozi wetu wanvyokumbana na maswali toka kwa wannchi wakiwasilisha kero zao, tumeona jinsi viongozi wetu wanavyopokelewa na mabango yenye vilio vya wannchi katika ziara zao.
Zamani walizoea kupokelewa kwa shangwe na ndereme huku wakiimbiwa nyimbo mbalimbli za kutukuzwa na kusifiwa. Lakini siku hizi mambo yamegeuka kabisa.
Swali la kujiuliza ni Je Uhitaji wa wananchi utapewa nafasi?
Kuna mikakati ya makusudi iliyoanzishwa na baadhi ya watawala hapa Barani Afrika ya kunyakua madaraka kwa kuiba kura na kama hilo likidhihirika, yanatengenezwa mazingira ya kuunda serikali ya Mseto.
Wote tumeona katika nchi jirani, serikali hizi za mseto hazina tija kwa wannchi na badala yake ni vurugu tupu, kila upande unataka kuonesha ubabe na hii huchelewesha kuwaletea wananchi maendeleo.
Muda mwingi unatumiwa na viongozi bhawa kutunishiana misuli na wananchi wanaachwa njia panda.
Mimi nina wasiwasi sana na hili nan ndio maan nadhani kuna haja ya kuangalia upya muundo wa Tume yetu ya uchaguzi.
Kuna haja kubwa sana ya kuunda Tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa haifungamani na upande wowote.
Mimi naamini kabisa kuwa tunao watu makini na wenye kuitakia nchi hii mema ambao wanaweza kusimamia uchaguzi kwa uhuru na haki.

Bado sijakata tamaa......