Saturday, August 1, 2009

Ungekuwa wewe ungefanyaje?


Najiuliza kama ungekuwa ni askari aliyekuwa akimfukuza na kujitahidi kumsimamisha "dereva" huyu na kisha ukatambua kuwa uliyekuwa ukimfukuza ni mtoto wa miaka 7 ungefanyaje? Ama kama ungekuwa mzazi wa mtoto huyu ungefanyaje? Ungemuadhibuje? Na pengine ungeaminije "ufundi" wa mtoto huyu katika kutenda alichotenda? Na je ungejiuliza kuhusu hatari iliyokuwepo huko Barabarani? Na vipi kuhusu mwanzo na mwisho wa tabia ya mwanao?
Na sasa najiuliza kama mtoto huyu atatokea kuja kuwa mkimbiza magari (mfano Formula One na Nascar) hawatahusisha tukio hili na "nyota njema iliyoonekana asubuhi?"
Najiuliza tu na ningependa kuiweka bayana hii CHANGAMOTO YETU ili tuelimishane.

7 comments:

Anonymous said...

Amenifurahisha kwa jinsi alivyoimudu barabara kama dereva mwadilifu, alichonifurahisha zaidi ya yote, ni vile alivyoshuka kwenye gari na kutimua mbio ha ha haaa.
Angekuwa mwanangu wala simchapi hata kidogo, ila namketisha chini na kumfunza kuhusu sheria na wakati anaoweza kuruhusiwa kuendesha gari kisheria. Kisha mpe michezo mingi ya kukuza kipaji chake cha uendeshaji na udadisi.
Watoto wanapenda kujua mambo mengi na kila wanapopata mwanya huwa wanajaribu.
Imekuwa rahisi kwake kuendesha hii kwa kuwa ni automatic, ingekuwa manual ingemsumbua kidogo tu lakini namfahamu mtoto mmoja mtaani kwetu alipakia trekta ya babake, manual, na kuiendesha mtaani akiwa na umri wa miaka 11 tu, kwa bahati mbaya alikufa kwa ajali ya pikipiki akiwa na miaka 21 tu (RIP).
Nimeipenda hii na hasa kwa kuwa haikutokea ajali, kama kutizama sinema vile, hapo mzazi wake lazima alikuwa kiroho juu. Bora haikutokea kwenye Highway.

Fadhy Mtanga said...

Mchangiaji da Subi amesema yote.

Zaidi ningempa big up kuuubwa, ila ningeweka maximum supervision kuepusha madhara.

Weekend njema.

Egidio Ndabagoye said...

Hiki kipaji kinatakiwa kiwe Ferrari.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

bahati mbaya sijaweza kuona hiyo crip naona kompya yangu inagoma kuonyesha

Mzee wa Changamoto said...

Da Subi. Huyu mtoto alikuwa na Video Games nyiiingi na kati ya hizo kuna iliyokuwa inafundisha namna ya kuendesha na kuwakimbia polisi ambayo inasemekana Baba yake aliichukua baada ya tukio hili (japo ameshaonesha uwezo wa kuendesha na kuwakimbia). Ikanikumbusha ile stori ya jamaa aliyekuwa akisafiri na pilot akafa angani wakauliza kama kuna mtu ana experience na kurusha ndege mmoja wao akasema ana masaa 300 ya uzoefu. Alipopewa urubani akaelekezwa cha kufanya mpaka akatua na baada ya kutua wakamuuliza hayo masaa amekuwa akirusha ndege za aina gani, akasema ni MASAA YA KWENYE VIDEO GAMES. Kwa hiyo labda zinaweza kukupa real skills kufanya jambo. Hivyo ni vema kuwa makini katika kuchagua games za mtoto maana zaweza kumfunza mambo ambayo wazazi hawana muda ama hawataki kumfunza.
Kwa hakika imekuwa ngumu kuamini kuwa mtoto huyu ameweza kulimudu gari na kuendesha katika mwendokasi huo wa 60mph na kuwakwepa askari katika namna aliyofanya. Siku moja baada ya hii clip kurushwa hewani alipata deal la kwenda New York na wazazi kuhojiwa kwenye Tv. Sijui usahihi wa hilo na nia ya kufanya hivyo kama ni kukuza kipaji, kuonya ama kuonesha nini kwa watoto wengine maana sijapata hiyo clip.
Kaka Fadhy umenena, kunahitajika supervision maana hii ingekuwa issue nyingine kama angekuwa sehemu iliyo busy basi tungeweza kuwa tunazungumza mengine sasa hivi.
Kaka Egidio. Asante kwa kupitia hapa na karibu saaana Kaka. Hiki sijui ndio kipaji cha kuzaliwa ama kufunzwa. Niliwahi kuuliza japo sikupata jibu na naamini ukitembelea makaa za nyuma kidogo unaweza kunisaidia kunyambulisha hili. Kama hiki ni kipaji na kama ni cha kufunzwa ama kuzaliwa nacho.
Kaka Kamala, najua baadhi ya compyuta huwa wanaweka settings zinazozuia kucheza videos za You Tube. Lakini najua wewe ni mtaalamu wa haya kwa hiyo utajua kama hili ndio tatizo ama la. Ama kama ni hii yangu inayogoma unaweza kui-search kwenye video webs naamini utaiona. Sikuweza kuipata kwenye webs za kawaida.
Sorry about this
Blessings yo ya'll

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

thanx nakwa kweli vyanzo vya tatizo hili ni vingi kikiwemo cha muda kupungua kuliko nitakavyo.

Anonymous said...

angekuwa mtoto wangu ningemchapa viboko ile mbaya ili akome na tabia hiyo ya hatari kwani angepata ajali na kufariki hapo ndio tungejua ni hatari lakini kwa kuwa kote amepita salama tunaona ni poa kabisa na bahati ni kuwa sehemu zote alizopita hajapishana na gari kwa hiyo mungu amemuepusha na ajali. kuna methali isemayo:-tahadhari kabla ya athari.mdau uk