Sunday, August 23, 2009

CHANGAMOTO YETU hiyoooo kambini...Tuonane NEXT IJAYO

Ndio niko Camp jamani
Jumanne ya Aug 25, blogu itakuwa ikitimiza mwaka mmoja. Ili kurejea kwa ARI MPYA, KASI MPYA na NGUVU MPYA, tumeamua "kupiga kambi" kujifua kurejea tena siku hiyo.
Tunataraji kuendeleza UELIMISHAJI, UBURUDISHAJI na UKOMBOZI WA KIAKILI kupitia maandishi na muziki.
Tunajivunia saana uhusiano wetu na wasomaji na wana-blog woote na kwa hakika TUNASHUKURU SAAAANA kwa kuendelea kututembelea.
Tukutane Jumanneeeeee ya tarehe 25 kwa AWAMU YA PILI
Na sisi tulikuwepo, na wao walikuwepo, na wewe ulikuwepo katika uelimishaji wa jamii
PamoJAH Daima

8 comments:

Fadhy Mtanga said...

Hongera sana kaka. Sitokuwa na zawadi kuuubwa siku hiyo, ntakachoweza, ntakuandikia tumistari tuwili tutatu pale kibarazani kwangu kama zawadi yangu. Usijisikie vibaya kwa kutopewa zawadi kuuubwa kama za mafisadi.

Yasinta Ngonyani said...

Nami pia natanguliza hongera zangu na. Na zawadi yangu itakuwa kukutembelea mara kwa mara

Simon Kitururu said...

Twaisubiri Jumanne! Naogopa kupongaeza kabla ya siku nasikia ni uchuro!:-(

Anonymous said...

Count me in, hiyo jumanne!
Hongera sana kwa kutimiza mwaka mmoja!

Upendo daima!

Unknown said...

hongera kaka, natarajia utaendelea kumwaga nyuki.....

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Tunasubiri!

Faith S Hilary said...

Many congrats kaka! I can't say no more just hongera.

PS: Kumbe una mwanya mduchu kama wangu hahahhahaha! jokin

Mzee wa Changamoto said...

Asanteni nyote. Kaka Fadhy, heshima kwako. Da Yasinta karibu kwa mara ya tena. Kaka Mkodo. Ni busara kuendeleza "nasikia" sometimes na kwa Kaka Mbilinyi. HESHIMA SAAANA NA ASANTE KWA UELIMISHAJI. Kaka Kaluse bado nakusoma Kaka na Kaka Matondo, TUKO PAMOJA.
AND FINALLY!!!!!!!!!
We Candy wewe!! Tabia gani ya kuchunguzana mianyani? LOL
Mie sina mwanya wewe, ni picha imekuwa scratched kidogo eneo la jino. Lol
Unaanza ugomvi eeeeeehh!! Nasubiri video yako na mie nikuangalie mwanya wako
NAWAPENDENI NYOTE