Friday, August 21, 2009

Happy Birthdate Glady

Kuanzia mwezi wa saba nakuwa an wengi wa kuwakumbuka wakisherehekea siku zao za kuzaliwa. Na kwa wale wenye kusherehekea ama kupenda kusherehekea siku muhimu nasi, nawakaribisha kuunganisha salamu zenbu hapa. Naamini tunaungana sote katika hili
Hey G.
Tangu enzi za Jitegemee mpaka sasa umeendelea kuwa Rafiki mzuri na mwema kwangu. Hakuna ninaloweza kukuombea zaidi ya maisha mema na mafanikio katika mipango yako yoote mizuri uipangayo na nakutakia maono makubwa na mazuri zaidi katika kupanga maisha yajayo.
Endelea kuwa mcha Mungu kama nikufahamuvyo na mchapa kazi kama ulivyo.
Heri ya Siku ya kuzaliwa.
Nasindikiza salamu zangu hizi za UPENDO na kibao ukipedacho saana cha DORE (Obugenyi)toka kwake Freddie Sebatta...
Happy Birthdate GLADY

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Heri G na uwe na diku njema ingawa nimechelewa lakini sidhani hongera hazitapokelewa.

Anonymous said...

Mzee, wallahi ushagaragaza wengi. Duh, we kiboko aisee. You appear polite lakini I smell danger. It is tru, Simba mwenda slow ndiye mla nyama! Mi nakuvulia kofia

Mzee wa Changamoto said...

We Anon wewe. Hebu fafanua maana ya KUGARAGAZA. Maana nashindwa kusema ASANTE kabla sijajua una maana gani. Unaongea kikwenu? Unaposema kugaragaza unamaanisha "kuwa na urafiki?" Kama ndio maana yake, basi nakubaliana nawe kuwa nimeshakuwa na urafiki na wengi. Ila kwanini nikiwa na urafiki wewe unuse hatari? Ama na hapa niombe ufafanuzi wa "I smell danger?"
Hebu rejesha hiyo kofia kichwani mwako na usinivulie kabla hujafafanua haya.
Lol
Karibu MFICHA JINA na nashukuru kwa kuendelea kuwa nasi. Nawe sema siku yako ya kuzaliwa ili tuweze kuwka hapa HAPPY BIRTHDATE ANON. (Ila utume na picha. LOL)