Friday, August 28, 2009

Happy Birthdate Kaka Rama Msangi

Ninawiwa furaha saana ninapoona mwendelezo wa chambuzi mbalimbali zinazoendelea katika magazeti-tando yetu. Na mmoja kati ya wale wenye lile tunaloliita JUKWAA LA UCHAMBUZI ni Kaka Rama Msangi.
Huyu amekuwa makini katika masuala ya blog na amekwenda hatua ya ziada mbele ya uandishi ambapo amefanya kazi njema kutengeneza blogu mbalimbali ambazo wengi wanaonekana kupendezwa nazo.
Leo hii sio tu NAMPA PONGEZI KWA KAZI AFANYAYO, bali pia kwa kutimiza mwaka mwingine kamili.
Ni siku anayosherehekea mwaka mwingine kamili katika maisha yake na hakuna tunalomtakia zaidi ya MAISHA MEMA YENYE MAFANIKIO KATIKA KILA JEMA ATENDALO.
Kazi zako zaheshimika, zakubalika na zaelimisha na tunaamini UTAENDELEA KUTUSAMBAZIA UJUMBE MWEMA KWENDA NA KUTOKA KWA JAMII YETU YENYE UHITAJI na kwa kufanya hivyo tutaweza kutimiza lengo letu.
HAPPY BIRTHDATE BROTHER RAMA
We all "OWE YOU NOTHING BUT LOVE, JUST LOVE.... STRAIGHT FROM THE HEART"
BLESSINGS

2 comments:

Simon Kitururu said...

Happy Birthday Mkuu!

Yasinta Ngonyani said...

Happy Birthday kaka Msangi!