Thursday, August 27, 2009
Them, I and Them....MHIMILI WA CHANGAMOTO YETU
Ni Mzee wa Changamoto na Jah Petes. Lead Vocalist wa Morgan Heritage
Moja ya sababu za kuanzisha Blog ilikuwa kuthaminisha na kukamilisha kazi kubwa ifanywayo na wengine ambao licha ya juhudi zao kuikomboa jamii, wameendelea kuonekana ni "uchafu" katika jamii hiyo.
Hawa ni watu ambao WANAIPIGANIA JAMII na kutaka kuielimisha kuondoka katika lindi la UJINGA NA UTUMWA WA KIAKILI. Wanafanya haya huku WAKIIBURUDISHA JAMII na kuiasa kuhusu walikotoka, waliko na waendako. Hawa ni wasanii wema wa muziki wa Reggae.
Binafsi nimekuwa "mlevi" wa hili kwa kuwa nimekuwa nikijiona ndani ya yale yaimbwayo humo na hakika JAMII IZUNGUMZIWAYO huwa inaendana zaidi na jamii yetu.
Katika mwaka mmoja wa maisha ya Changamoto yetu, tumeweza kushereshana post 50 zan kipengele hiki na japo zooote zinaigusa jamii lakini zipo ambazo mpaka leo nikizirejea najiuliza "KWANINI WENYE KUELEZWA HAWAYASIKII NA KUYATENDEA KAZI HAYA"?
Labda najihisi hivyo kwa kuwa ni mazungumzo kuhusu JAMII INAYOKANDAMIZWA ambayo mara zote nimekuwa nikiifikiria.
Na leo nimeona niziweke hapa post hizi wakati tunamaliza wiki ya "kuangalia nyuma" na kuanza awamu ya mwaka wa pili.
KWA WATOTO.
Hawa wamekuwa wahanga wakuubwa saana wa matatizo ya jamii. Hawajui hata pa kukimbilia na kibaya zaidi hata wanapolazimika kukimbia hawajui kwanini wanalazimika kukimbia na hawana uhakika wa kuwa wakimbiliako ndiko kuliko na usalama. Wanauawa bila kujua tafsiri ya serikali wala maisha mema ambayo tunaambiwa kuwa wapiganao wanawatengenezea. Kwa ujumla niliandika kuhusu maisha yetu na uhitaji pamoja na utambuzi wa wale WANAOTUTAWALA (Bofya hapa kujikumbusha) ambayo kwa hakika UKISOMA NA KUWASIKILIZA WASANII wnaeleza yote. Lakini tugusapo JAMII kwa ujumla, basi lazima tutaongelea utawala. Na mara nyingi nimesema kuhusu WATAWALA WETU NA MAAMUZI YAO yasiyo na mwelekeo.
Kibao ninachosikiliza zaidi ni hiki chake Lucky Dube kinachoonesha namna ambavyo HESABU ZA KISIASA zinavyoweza kutojali uhalisia wa maisha ya walengwa. Ni kibao SOLDIER (Kisome hapa) ambacho kitakwimu chafuatiwa na kile chao Morgan Heritage nilichokiandikia siku chache kabla ya Sherehe za Uhuru. Hiki chaitwa NOTHING TO SMILE ABOUT (Hapa) ambacho ni kama kinaeleza UKWELI WA YAENDELEAYO NCHINI MWETU.
Magonjwa, Rushwa, Ufisadi, Maisha mabovu, Ukwiukwaji wa haki za binadamu, uwiano m'bovu wa walio na wasionacho, matabaka, mauaji, imani za kishirikina, siasa chafu, UTAWALA usiojali mahitaji ya wananchi na mengine mengi. Haya yote tunapoyaangalia twaishia kujiuliza kama sifa tupewazo na kuzisikia nje ya nchi kuhsu Tanzania zamfaa kwa namna yoyote Bibi yangu kule Kihanja ama mtu wa Rubafu au Nangurukuru ambaye yawezekana hata hajui kuwa serikali inastahili kumpatia MAISHA BORA.
Mwaka mpya unaanza wa pilika na mipango mipya katika kuifanya jamii iwe mpya ikiwaza upya kuijenga upya Tanzania.
Yawezekana kama tutashirikiana na mhimili huu wa blog utaendelea kuielimisha jamii. Mtu mmoja mmoja kwa wakati.
Blessings
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
6 comments:
nimeifagilia andiko katika nguo uliyoivaa. naomba utaratibu wa kupata ngua yenye andishi kama hiklo ndugu na ikibidi litafisiriwe kwa kibongo.
unanisaidiaje?
Umesema kweli hakuna mtu anayesikia na kama wanasikia basi hakuna utekelezaji.Kunahitajika mabadiliko. nimeipenda hiyo ramani ya afrika(culture) ....LOL
Usijali Kamala. Ntajitahidi kufanya hilo. Hiyo nilipeleka neno kwa mtengenezaji akanichapishia. Kisha nikaamua kutumia neno hilohilo kuweka hapo juu kama kichwa cha blogu. Kutengenezesha si tatizo hata kidogo. Naamini hiyo ntaweza kumudu gharama na nikipata ajaye huko, ntawasiliana nawe kukupa lenye tafsiri ya Kiswahili.
Tutawasiliana kwenye e-mail kujua ukubwa upendao
Da Yasinta. Nashukuru kwa kuendelea kuwa "yule yule" siku ile, sasa na pengine hata kesho na mtondogoo. Lol
Nuff Respect
Kaka ipo siku tu somo litaeleweka, cha msingi ni umoja wetu,mshikamano wetu, tutafika tu,together as one,hata mmea wa kabichi, kama majani yake hayataungana basi kamwe kabichi haitapatikana.
asante
Sijui kwanini nimekusoma halafu nikajikuta nafikiria kazi ya YESU a.k.a Nabii Issa ambayo eti nayo baadaya miaka yote hii TOKEA AANZISHE eti nayo bado walengwa hawajaisikia:-(
Post a Comment