Tuesday, August 11, 2009

Kipi chazeeka kwanza, miili ama akili??????

Nikiwa kazini na "rafiki" yangu (ambaye ana umri mkubwa), tulikuwa tukiongelea jinsi watu wanavyoukimbia muonekano wa umri wao. Na yeye alionekana kutetea hilo na kusema kuwa awali alikuwa akionekana ana mvi nyingi kichwani na alijihisi MZEE. Lakini baadae akapata dawa ya kubadili rangi ya nywele zake na hilo likamrejesha katika "ujana" aliokuwa akiutaka. Na baada ya kuonekana kuwa kijana zaidi, akaanza kujihisi kuwa na hata nguvu na uwezo wa kufanya mazoezi. Sasa hivi anakimbia dk 30 za mapumziko ya mchana kazini na amebadili mfumo wake wa chakula, amebadili mfumo wa maisha na kwa hakika sasa anaishi "maisha ya afya" zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Hakuna anayebisha kuwa KUJIONA KIJANA kumemsaidia kubadili mfumo mzima wa maisha. Lakini kwangu swali likabaki kuwa alizeeka mwili ama akili? Ni kweli kuwa kabla hajajiona kuwa kijana zaidi mwili wake usingeweza kutenda mazoezi afanyayo sasa? Na je! kama angekuwa amezeeka mwili, angeweza kutenda atendayo hata kama angekuwa anapenda kufanya hayo?
Ninawaona wengi ambao kwa kujiona "wamezeeka" hawajiendelezi na shule, hawawekezi maishani na hata hawafanyi mengi mema ambayo yangewasaidia miaka michache ijayo. Wanaokimbia vivuli vyao kwa kujifanyia upasuaji kutafuta muonekano wa ujana, kutumia makemikali "kijijananisha" na hata kuvaa ki-ujanaujana wakiamini hilo litawapa HISIA nzuri za namna walivyo. Pengine inawasaidia kwani wapo ambao wakishakuwa katika "ujana" wautakao huanza kutenda yale ambayo ni ya manufaa kwa maisha yao na zaidi kwa wale wategemezi wao lakini ambayo wangekuwa wamefanya ama walistahili kuyafanya kabla "hawajajibadilisha."
Haya na mengine mengi hunifanya nijiulize tena na tena.
KIPI CHAZEEKA KWANZA? MIILI AMA AKILI?

6 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

swali zuri japo kuna uzushi mwingi hapa. wengi tunaishi maisha feki na yasiyoharisi kwa kuukimbia uhalisia wetu. mojawapo ya sababu kwa nini tunaendelee kurudi duniani (ku- reincarnate) ni kwa sababu hatujaweza kuhuhishi uhalisia. yaani hatujaweza kuishi maisha yetu halisi tupaswayo kuyaishi hapa duniani na badala yake tunahaingahika tu kwa vitu visivyo hitajika kwetu wala kwa Muumba.

mpaka tujikubali na kujipokea. tunajali sana ya nje yetu kwaba fulani ananionaje badala ya sisi tunataka tuweje au tujioneje. kuzeeka ni muhimu na lazima tukubali. kwa hiyo kama huyo rafiki yako kazeeka akili au zimeshakufa na labda hazijazaliwa.

kwenye ulimwengu wa kiroho (science of the soul) hakuna uzee wala ujana kwani kizeekacho na kuchakaa ni mwili tu na sio sisi halisi.

nimechoka kutaip bwana ila nimeeleweka.

chib said...

Swali gumu, lakini nafikiri linategemea vinasaba (genetics) na mfumo wa maisha ambao mtu anaishi. Kwa mtazamo wangu mwili huzeeka haraka kuliko akili, kadiri unavyozidi kuwa mrefu sana na ndio mwili huzeeka mapema zaidi.Sina ushahidi wa kisayansi isipokuwa nazungumzia kwa uzoefu

Fadhy Mtanga said...

Hili ni darasa. Naendelea kupiga shule.

Yasinta Ngonyani said...

Kwa mtazamo wangu hii inategemea kwa kila mtu. Wengine huanza kuzeeka miili na wengine akili.

Faith S Hilary said...

Yah inategemea na mtu na vilevile the way you live your life, I saw on Oprah show babu wa miaka 92 bado ni heart surgeon, bibi yangu alikuwa na miaka 98 na bado anajua yupi ni yupi, anaanika machicha ya nazi, anaosha vyombo e.t.c (RIP to her by the way), so inategemea japo sina mfano wa mtu kuzeeka akili kwanza kabla ya mwili...

Albert Kissima said...

Stress katika maisha zaweza kusababisha akili kuchoka mapema hata na mwili vilevile ila kuchoka kwa mwili kunategemea hasa stress mtu anazipokea namna gani.

Mtu anaweza kukusimulia matatizo yake na ukastaajabu kwani ukimwangalia kwa nje huwezi kudhani angeweza kuwa na matatizo aliyosimulia.


Watoto wa mitaani, miili yao yachakaa mapema kwa kukosa matunzo.Hawafikiri kuhusu maisha yao.Laiti wangeweza kufikiri juu ya mustakabali wa maisha yao,wangeumiza vichwa au wangefikiri kushinda uwezo wao juu ya mazingira waliyonayo na wangeathirika kimwili na hata kiakili.

Je wapata picha gani pale ambapo mtoto anapoambiwa hatakiwi kuwa na mawazo kwani yeye bado si mtu mzima?

Watoto wanaolazimika kuwaza kutokana na changamoto zinazowakabili, akili zao hazilazimishwi kuzeeka?
Ni hayo tu.