Monday, August 10, 2009

Ni mwaka mpya kwangu. Ni siku yangu. Asante kwako

Siku zinasonga na kwa hakika licha ya ugumu tupitiao, tukiangalia nyuma twaona kama jana tuu tulipokuwa tukicheza kama watoto.

Nami sasa nimetulia kuangalia maisha yangu yaliyopita katika siku hii ninayokumbuka kuzaliwa kwangu. Na ninajifunza mengi kwa kukumbuka mengi. Najua maisha yangu yasingekuwa yalivyo kama nisingezungukwa na watu niliozungukwa nao. Labda ningekuwa na watu tofauti ingekuwa zaidi ya hapa ama pungufu yake, lakini kwa sasa sina la kulaumu bali NASHUKURU KUWA NILIVYO.
Kwa hakika kuna wengi waliogusa maisha yangu ambao kwa namna moja ama nyingine wamebadili maisha yangu. Huwa nawafikiria saaana na mara kwa mara nimekuwa nikijaribu kuandika chini watu hao ili niweze kuwashukuru kwa pamoja lakini nimeshindwa. Tarehe 7 Aprili nilijaribu kwa mara ya mwisho kuwashukuru wote lakini nikashindwa na ndio chanzo cha kuandika kuwa HUWEZI KUWAHUKURU WOTE, WAOMBEE TUUU (Bofya hapa kusoma).
Kila mmoja ana nafasi ya pekee kwangu. Kwa wanafamilia yangu sina la kusema. Wakubwa mmekuwa mkinionesha njia kwa upendo na unyenyekevu na mara zote kunisaidia pale niangukapo na wale wadogo kwangu mmekuwa mkinitia moyo pale nilipoonekana kukosa wa kuwa upande wangu. Shukrani kwenu. Kwa wale tuliocheza wote, furaha tuliyokuwa nayo wakati huo ndio chanzo cha fikra za sasa. Tuliosoma wote, bila ninyi nisingeweza songa mbele kwani mlisaidia kwa namna kubwa saaana na wale niliofanya nao kazi na hawa tunaoendelea kufanya kazi ya kuielimisha jamii na zaidi wale wasomao hapa kusaidia kunielewa, NAWAPENDA SAAAANA.
Labda nitoe upendeleo kwa watu watatu. Mmoja ambaye licha ya kuthamini mchango wake kwangu na kumuombea kila leo, bado nahitaji msaaada wa kuwasilaiana naye. Si mwingine bali ni RENATHA BENEDICTO ambaye niliandika habari ya kumtafuta HAPA (bofya kuisoma) na bado naendelea kusubiri mawasiliano naye.
Wa pili ni KAREN ambaye amekuwa na support ya aina yake maishani mwangu
MWISHO NI SALAMU ZA UPENDO KWA WANGU WA PEKEE Esther. NAKUPENDA SAAANA, NAKUHESHIMU, NAKUTHAMINI NA NAPENDA UTAMBUE KUWA UWEPO NA USHIRIKIANO WAKO MAISHANI NI KATI YA VITU VYEMA NINAVYOJIVUNIA KATIKA MAISHA. SINA LA ZIADA NINALOWEZA KUMUOMBA MUUMBA
Ni mwaka mpya Kwangu, Ni siku yangu na ASANTE KWAKO
THANK YOU LORD

16 comments:

Faith S Hilary said...

Hongera kwa kusherehekea siku yako ya kuzaliwa na Mungu akubariki uishi miaka mia kidogo. Love the video which was great taking us through your life by images. Once again hongera kaka. (Nibakishie keki) lol

Anonymous said...

Heri kwa sikukuu ya kuzaliwa. Mungu akujalie heri ya maisha mema na afya njema katika siku alizokujaalia uhai hapa duniani.

Fadhy Mtanga said...

Heri ya siku ya kuzaliwa kaka Mubelwa.
Maisha yana tafsiri nyingi kutokana na vile mtu anavyoishi na aina ya watu anaokutana nao.
Kwako, nakuombea maisha yako kuwa marefu yakiwa ni yenye upendo, furaha tele na mafanikio.
Hongera sana kwa siku hii muhimu.

Koero Mkundi said...

I send to you warm wishes,that your happiness will be as wonderful as the happiness, you have always given me. wish you happy birthday my Bro......

QUOTES:
Very few people do anything creative after the age of thirty-five. The reason is that very few people do anything creative before the age of thrity-five.
- Joel Hildebrand

SHABANI O. KONDO said...

KAKA HONGERA SANA KWA KUFURAHIA SIKU YAKO YA KUZALIWA KI UKWELI NI BAHATI ILIOJE KWA KILA MWANAADAMU INAPOFIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA KAMA ILIVYO KWAKO.

LAKINI KAKA SIJAFAHAMU UMEFIKISHA MIAKA MINGAPI? NI VYEMA UKATUJUZA WADAU.

HEPI BNESDEI KAKA.

Yasinta Ngonyani said...

Nikikutumia au litasinyaa, kadi itachakaa, msg utafuta. Nakuombea SALA,Mungu akubariki, akuongoze akusaidie ktkt mambo yako yote. Hongera sana kwa siku hii muhimu yaani kwa kuongeza mwaka.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

interesting hata kama hujatundika picha za enzi zile unakula sifuri ukiwa bado sifuri bila kujua tofautia ya chakula na mchanga au uchafu au enzi zile mwili wamama yako ukiwa chanzo muhimu cha chakula chako kupitia maziwa.

tunakumbuka mengi na jua kusheherekea birthday ni kukukmbuka kuwa kuna kifo, je utakufaj na uende wapi?

happy birthday na nimeshangaa kuona una mdogo aitwaye BinaOmutonzi!!!

usile keki kwani kuna mayai ndani.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

watoto ni malaika na ukiangalia picha yako ya udogoni, basi wajiona ulivyo kuwa mzuuri unapendeza na unavutia. ndivyo ulivyo hata leo na wote waliokuzunguka ndivyo walivyo. ni wazuri kama picha zako za ujingani a.k.a umalaikani a.k.a udogoni. hata wanyama, mbwa paka, wadodo hata ngombe, wanapendeza, achana kabisa na tabia ya kuwatafuna kwani ni wazuuri pia. ila kuna chakula maalumu kwa ajili yako./

waonaje ukiangalia embe bivu au chungwa au viazi na mihogo? vyakukaribisha, njoo unile niko tayari kwa ajili yako. unaviacha na kukimbizana na wanyama ili uwaondolee uhai na uwatafune, badilika birthday hii ndugu.

hata hivyo, umekua, HAPPYBIRTHDAYY mzee wa Moto Changaz

chib said...

Congrats!! :-))

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Happy Birthday. Umeinukia kuwa mpiganaji na mwelimishaji bora wa jamii yetu. Usije ukaliacha pigano.

Baraka Mfunguo said...

Happy Birthday natumai libeneke linazidi kupendeza. Kila la heri

Unknown said...

HAPPY BIRTHDAY KAKA, BLESSINGS!!!!

BC said...

Kwanza hongera sana kwa kusheherekea siku yako ya kuzaliwa,siku ulipokuja katika dunia hii ambayo,kwa bahati mbaya sana,sote tu wapitaji tu.

Pili,lazima nikupe hongera kwa jinsi ulivyotengeneza hiyo video.Hata nisingekuwa nimesoma ulichokiandika mwanzo,ningeelewa kabisa historia nzima.Ni mikasa,mihangaiko na mafanikio.Hongera kaka.Nakutakia kila la kheri.

Mzee wa Changamoto said...

Ni ninyi wapendwa mnaonifanya niwe nilivyo. Mmekuwa msaada mkubwa kwangu na NAWASHUKURU SAANA.
Nawaombea kila lililo jema na naamini kwa PAMOJA TUTAISAIDIA JAMII KUSONGA MBELE
Blessings

Nicky Mwangoka said...

Happy Birthday Kaka.You are a great person of our age, May the Good Lord grant you strenth and wisdom to keep on neing the light to this current world. Big up Brother. We are together in Thanking God for the gift of life in you

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Naamini hakuna kuchelewa katika kutiana moyo na kutumia salamu.

Nakutakia kila jema na mafanikio katika mchakato mzima wa maisha.

Tupo pamoja ndugu yangu..

Ujumbe wangu kwako " God's able"

...
Ndaki wa Edo