Friday, August 14, 2009

Them, I & Them...2Isis.....Ghetto Pain

Sijui ni uchovu ama mawazo ama maumivu ama matumaini ama...... Najua ana REAL GHETTO PAIN
"Mjasiriamali" akitolewa mahali "anapochafua" jiji...Wenye nacho wanasema hawa wanachafua jiji na kuwaondoa ni kulipa jiji "hadhi". Japo "walikaribishwa" na hawajapangiwa pa kwenda Bweni. Shule ya Sekondari Zingibari Tanga
Mtihani wa Mock, darasa la saba S/M Maendeleo Mbagala Kuu DSM. Hii ni Dar, Mwendo wa masaa machache kutembea kufika Ikulu, sijui Kyamalange ama Nanjilinji kutakuwaje?
Bungeeeeee!!! Hahahahaaaaaaa
Posho za kukaa "mbinguni" humo
Katika vitu vinakera nchini mwetu ni namna tunavyjitahidi kutatua tatizo kwa kuzuia ZAO LA MWISHO LA TATIZO HILO NA SI MWANZO WAKE. Nchi inajitahidi kila leo kuwafukuza wamachinga kuwapeleka ambako haijawaandalia mazingira mazuri ya biashara na ambako hakufikiki kwa mwananchi wa kawaida. Inajitahidi kuwahimiza vijana kurejea vijiji / kutokuja mjini wakati inazidi kudimimiza vijiji na KUWANYONYA wanavijiji wengi. Serikali inayohimiza elimu wakati wanafunzi wengi wanasoma katika mazingira magumu zaidi ya jela (Huamini? Angalia TAIFA LA KESHO hapo juu kisha Bofya hapa uone jela inayozidi taasisi zetu za elimu) . Ni juzijuzi serikali imeanza kuzungumzia mkakati wa kufundisha Kompyuta nchi nzima. Utaziweka wapi wakati wanafunzai wanasoma na wengine "wanalala nje"?Mazingira kama yaoneshwayo hapo juu hayampi mwanafunzi nafasi ya kufikiria masomo zaidi ya kumjengea UJASIRI WA HOFU na kumkomaza. Labda kama lengo ni kupata maKOMANDOO.

Ni serikali yangu Inayohimiza USAWA kwa wote ilhali ina watumishi wanaofanya maamuzi kwenye JUMBA lenye hadhi zaidi ya kazi wanazofanya (sio wanazotakiwa kufanya), kupata mshahara wasiostahili na kuwatelekeza wanaolitumikia taifa kwa moyo mkunjufu na kwa muda mrefu. Serikali inayohimiza maendeleo ilhali wanaomaliza shule hawaajiriwi kwa kuwa hakuna pesa wakati pesa WANAYOKOMBA wao wabunge ingeweza kuendeleza sekta kadhaa kwa kuajiri wenye ufanisi wa kazi.

Wengi wa wabunge wetu HAWATEMBELEI MAJIMBONI baada ya kuchaguliwa na kwa kuwa wana kila wanachohitaji, hawana haja ya kujijaza msongo wa mawazo (stresses) kwa kujua ukweli wa ugumu wa maisha wa watu ambao hawana huruma nao. Lucky Dube (ktk wimbo wake Crime and Corruption) alimuuliza KIONGOZI kuwa "Is it the bodyguards around you? Is it the high walls where you live? Or is it the men with the guns around you twenty four hours a day that make you ignore the crying of the people?"

Mpaka lini wananchi watalia juu ya unyanyaswaji utokeao, juu ya rushwa iendeleayo kuteketeza maisha ya wasio nacho, juu ya ugumu wa maisha wasiostahili, juu ya athari za RASILIMALI badala ya faida??????

HAKUNA ANAYEJUA MAUMIVU YA MAISHA TUNAYOJITAHIDI KUYAKIMBIA KWA KUWA WENGI WAO HAWAJAWAHI KUYAISHI.

Kwa maana hiyo, hawaijui ile tuiitayo GHETTO PAIN. Wacha 2Isis wawaeleze.

Verse 1
From day to day we live
Searching for our identity
While
the rich man says
We are a menace to society

But they dont know what its like (they dont know)
What its really like
What its really like

Chorus
To face real ghetto pain
To face real ghetto pressure
To face real ghetto pain
To face real ghetto pressure


Verse 2
On and on we go
For it we try to uphold
Our brothers turn to crime
Killing each other for a dime
While the opressor say
That turnin to qualities

Is the only way


Chorus
We face real ghetto pain
we face pain pressure
we face real ghetto pain
we face real pressure

Bridge
One day one day the table will turn
And to all me out there (to all me out there)
Beware for our barriers will burn (burn burn burn)

Verse
On and on we go
For it we try to uphold
Our brothers turn to crime
Killing each other for a dime
While the opressor say
That turnin to qualities
Is the only way

Chorus

Repeat Bridge, Verse 3 and Chorus


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
Picha: Mtaa kwa Mtaa, Global Publisher, Matondo Blog, Faustine Baraza.

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

visit here to see the reality

http://kamalaluta.blogspot.com/2009/08/maisha-bora-yashafika-hamyaoni.html


kuna wakati mambo hupendeza

Albert Kissima said...

Inasikitisha,inafedhehesha.
Najiuliza kama wananchi wanayaona haya,mitihani inafanywa ktk mazingira ambayo hata kama mwanafunzi anajua atafeli tu kwa sababu mazingira hayafai.Hela ya pango la spika tu yatosha kujenga bweni zuri la kisasa kabisa.
Kwa hali hii naona hata kwa kura mizizi hii haitaweza kung'olewa,watapigiwa wengine,na watatangazwa wengine kuwa ndio washindi,ni vema tujiulize kama hali hii ikitokea tutafanya nini? Hata hivyo kwa mind zetu zilivyokuwa corrupted, hata tuliowachagua wenyewe wasipotangazwa kuwa ni washindi, tutaona shwari tu na tutasema ni bora kila mmoja anaishi na bila kujiuliza kila mmoja ataishi vp.
Matokeo yake maisha yanakuwa magumu hadi kufikia hatua ya kuwindana kama wanyama,mauaji ya albino ni mfano hai, ujambazi unaogharimu maisha ya watu kila leo ni miongoni mwa matokeo ya uongozi mbovu.DA!

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli inasikitisha sana

Nicky Mwangoka said...

kaka hizi taswira ni nzuri sana na zinatafakarisha mno. Yaani viongozi wetu wangekuwa na macho na moyo wa tafakari wangeona haya na kuyafanyia kazi.