Friday, August 7, 2009

Them,I & Them......BUSHMAN.....Give Me Some More

"Politicians are the same all over. They promise to build a bridge even where there is no river. " Nikita Khrushchev (1894 - 1971)
Wiki hii inaelekea kuisha, lakini kwa mTanzania wa kawaida, ni wiki nyingine yenye machungu maishani mwake.
Wiki hii tumeendelea kusikia kuhusu ajali zinazoendelea KUIMUNG'UNYA jamii yetu bila kuwa na jitihada zozote za kuzuia ongezeko hilo. Kwa mujibu wa Blog ya Dr Faustine, "Hivi karibuni serikali ilitoa tamko ikisema kuwa licha ya ajali hiyo, tayari watu 1,468 walikuwa wamekufa na wengine 8,373 kujeruhiwa katika ajali 10,168 za barabarani zilizotokea nchini katika kipindi cha Januari na Juni, mwaka huu." Hizi namba zinaweza kumkosesha usingizi yeyote aliye katika mamlaka na serikali yenye kujihusisha na kujali maisha ya watu wake.
Nimeshuhudia mfanyakazi wa serikali aliyeitumikia kwa uadilifu akitumia zaidi ya nusu mwaka kufuatilia mafao yake ambayo ameyatumikia kwa takribani miongo 3. Sijui kama wabunge hawajaanza kupokea pesa kwa kiwango kipya cha mishahara walichojipatia. Na hapo hatujazungumzia waleeeee wa Jumuia ya Afrika Mashariki ambao wanahaha kufuatilia HAKI YAO.
Sijui ni lini WANASIASA WETU watakapotambua kuwa kazi waliyoajiriwa na wananchi ni kusaidiana nao kuijenga nchi?
Ijumaa ya leo ninarejea kwake Bushman katika wimbo wake Give Me Some More ambao niliuandika Jan 23 (angalia toleo hilo hapa) akiwaeleza wanasiasa kutoa kwa wananchi badala ya kuwanyonya. Tumesoma yalivyo matumizi ya Spika (YASOME HAPA) yaliyonifanya nikubaliane na Bushman anaposema "Tell me when will some clothes be issued to the naked, tell me when the hungry will be fed, tell me when will some shelter given to the homeless, ... can't you see the're dying there?" na kisha akaendelea kuimba "cause the ones who are suppose to make it easy, are the same who are making it harder"
Sijui kitakachowaachisha hawa wanasiasa kutenda watendayo, ama kitakachowafanya wananchi kuonesha wamechoka. Lakini kwa leo NAWAASA wanasiasa kutekeleza waliyoahidi na ku-give some more to the poor
Msikilize Bushman katika wimbo huu. UKISIKILIZA KWA MAKINI KUNA MENGI YA KUWAELEZA WAHUSIKA.

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

politicians and politics, ohhh mmmy GOD

Fadhy Mtanga said...

Kwa sababu wanaopaswa kuyafanya mambo rahisi,
Ndio hao wanaoyafanya kuwa magumu.

Inafikirisha, ikimaliza inaumiza.

Simon Kitururu said...

DUH!:-( Asante kwa hii na siku njema Mkuu Mubelwa!

Yasinta Ngonyani said...

Mi sisemi kitu leo ila tu nasema Ijumaa njema.