Sina hakika ni wangapi wameshausikia wimbo huu ONE TIN SOLDIER ambao uliimbwa miaka ya 1960 na ambao ni utunzi wao Dennis Lambert na Brian Potter. Kama umeusikia unaweza kuwa umejiuliza maswali mengi kuhusu maana yake. Nimeusikiliza mara kadhaa na kujiuliza kama yaliyoimbwa (ama niseme kutabiriwa) miaka hiyo ndiyo tuyaonayo hivi sasa nchini Tanzania? Wimbo unazungumzia watu wa "Mlimani" na "Bondeni" ambao kwa pamoja wanajua kuwa kuna "MALI YA THAMANI" iliyozikwa mahala lakini hawajui ni nini. Na kwa kuwa kuna UROHO wa kutopenda kugawana mali hiyo, wale wa "bondeni" wanapoomba kushiriki katika umiliki wanahakikishiwa hilo lakini wanaishia kuuawa wanapokwenda kuiona kama walivyoahidiwa na wa "mlimani". Na baada ya "kuwafyeka" walke wa bondeni, watu wa mlimanbi wanakwenda kufunua ilipo mali hiyo ili kujimilikisha na wanakuta HAZINA iliyopo inaomba AMANI DUNIANI lakini hiyo ni baada ya kuwa wameshatenda mauaji na kuwateketeza wenzao. Katika kufananisha nielewavyo mimi na "wachambuzi" wengine, nimekutana na mmoja wa walioelezea maana yake akisema na hapa nanukuu kuwa "That greed won't get you anywhere and that betraying your friends will ultimately leave you with nothing but loneliness." Sijui ni lini viongozi wetu watalitambua hili na kuacha "kuwaangamiza" wananchi wakitaka kujilimbikizia mali zisizodumu? Kaka zangu Kaluse na Kamala wameandika na kuzungumzia saana juu ya hili lakini WATAWALA wetu wameamua kufunga macho na kuziba masikio.
Ukiusikiliza na kuusoma unaelewaje? Fuatilia wimbo huu katika toleo hili lililoimbwa naye Bushman.
"Listen people to a storyUkiusikiliza na kuusoma unaelewaje? Fuatilia wimbo huu katika toleo hili lililoimbwa naye Bushman.
that was written long ago,
Bout a kingdom on a mountain
and the valley folks below
On the mountain sit a treasure,
buried deep beneath the stone
And the valley people thought
they'd have it for their very own.
Go ahead and hate your neighbor,
go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven,
you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing,
On the judgment day
On the bloody morning after,
one tin soldier rides away.
So the people of the valley
sent a message up the hill
Asking for the buried treasure,
tons of gold for which they'd kill
Came an answer from the mountain,
"with our brothers we will share
All the secrets of our mountain,
all the riches buried there."
Now the mountain cried with anger,
"Mount your horses, draw your swords"
And they killed the valley people,
so they won their just rewards
Now they stood beside the treasure,
on the mountain, dark and red
Turned the stone and looked beneath it,
"Peace on earth" that all it said.
Go ahead and hate your neighbor,
go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven,
you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing,
On the judgment day
On the bloody morning after,
one tin soldier rides away.".... x2
5 comments:
Kaka nimejifunza kuwa tatizo si kwamba hawasikii. Tatizo ni kuwa wanasikia sana isipokuwa wanajipa moyo kuwa kelele za chura hazimzuwii tembo kunywa maji.
Yeah funzo nililolipata hapa kwanza ni la wale ambao wanahodhi madaraka yao kwa kutumia migongo ya wananchi, halafu wao kujiona kwamba madaraka hayo ni haki yao kwa kumtoza mwananchi kodi,kutokuwa na mipango ya uhakika, rushwa,ukosefu wa huduma muhimu katika jamii, vifo, unyanyasaji. Katika kundi hili watu wa bondeni ni sisi wananchi wakati hao wa milimani wao wanabuni mikakati na mbinu za kung'ang'ania madaraka mfano mifuko ya majimbo ambayo haina manufaa kwa wananchi. Baadae wanapokuja kutaharuki uchaguzi umewadia na wamesahau mambo ya msingi waliyokuwa wakipigiwa kelele. Wimbo huu umenigusa sana
Mimi nafikiri wanasiasa wa kwetu hawakai hata hapo mlimani, maana kukaa mlimani maana yake kuna mapambano, ambayo yanaweza kuwatimulia vumbi. Wao kimsingi wanaishi kwenye ndege hewani kwa gharama za wananchi na kushuhudia wamlimani(vibaraka wao) wanvyowafyeka wanotokea bondeni (wananchi). Na mwisho wa siku wakati vibaraka wao wapo hoi, basi hushuka na kujizolea.
Amini usiamini, maisha ya wanasiasa ni ghali sana, lakini wanajizolea kila siku kwenye ma tume nk
kaka mie naomba nikalale nikichemsah bngo kesho natoa jibu la uhakika hapo maana duh si unajua kumpiga chura teke ni kumuongezea hatua?
dada yako hapa malkia wa bambataa
sophie.
Mzee wa Changamoto
Nimependa sana ujumbe huu.Lililoimbwa hapo ni kweli kabisa.Utajiri huja na maringo,majivuno,dhihaka nk.Lakini swali ambalo wengi hatujiulizi ni je ukiwa peke yako hapa duniani,utaringa?Utajivuna?Hapo ndipo ninapoliangalia upya lile azimio la mwalimu...la pale Arusha.Bado sioni makosa mengi hususani nikizingatia nyakati.
Post a Comment