
Yaonekana KUONGOZWA NA UTASHI WA MWILI ni tatizo kubwa kwani kutokana na tofauti za mahitaji ya miili yetu tunajikuta TUNAENDELEA KUJIPOTEZA KATIKA HARAKATI ZA KUJITAFUTA (Isome)
Ndio maana JUMATATU ya leo naungana na wana Msondo ngoma katika kumuomba MOLA kuirejesha dunia iwe kama ile ya zamani.
Ndani mwake utamsikia Maalim Gurumo akiimba "imani na upendo duniani vimetoweka, ufukara na umaskini vimetawala"
Wasikilize wana Msondo.
Tx Moshi William, Othman Momba, Joseph Maina na Seleman Mwanyiro ni baadhi ya walioshiriki ktk wimbo huu ambao wameshatangulia mbele ya haki. MPUMZIKE KWA AMANI NA KAZI YENU YAENDELEA KUELIMISHA
** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**
1 comment:
Ni kweli kabisa sasa binadamu wa sasa wamekuwa wakatili sana. Sasa sijui watu wa zamani walitumia mbinu gani ambayo sasa inashindwa kutumika? Asante sana kwa zilipendwa nimekumbuka nilipokuwa kachiki. Lol
Post a Comment