Sunday, September 20, 2009

Eid Mubarak

Kama kuna jumuisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, basi ni mafunzo ya KUMREJEA NA KUMTEGEMEA MUNGU katika maisha yetu ya kila siku. Nami napenda kuungana na wale wote waliofunza na kufunzwa kwa mawazo, maneno na matendo juu ya umuhimu na uwezo wa Mungu katika maisha yetu na naamini kuwa yale mema tuliyofunzwa yataendelea kukaa nasi maishani na kuwa sehemu kubwa ya maisha yetu.
Nawatakia wote siku njema ya Eid na naamini tutaendeleza mema katika maisha yetu kama ambavyo tumekuwa tukifanya katika mfungo wa Ramadhani.
Blogu ya Changamoto Yetu inawatakiwa wooote Eind Njema na tunaomba tuzidi kushirikiana katika kuielimisha jamii kumtegemea Mungu na si mali zetu ama za wenzetu, nafasi zetu ama nafasi za wenzetu, na hata mfumo wetu wa maisha ama hata mifumo ya wenzetu.
Basi tutende kama kadi isemavyo kuwa "tukimuita yeye (Mungu) atajibu sala zetu"

Eid Mubarak

6 comments:

Koero Mkundi said...

HE! KUMBE MWEZI UMEONEKANA.....
JAMANI IDDI MUBAAKA WANBLOG WOTE POPOTE MLIPO....

Mzee wa Taratibu said...

EID MUBARAK KWA WOTE SHUKRAN.

Albert Kissima said...

Furaha, amani na upendo vitawale miongoni mwetu.

EID MUBARAK kwenu wooote.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ALAHHHHHHHHHHHHHH AAAAKKKBARRRRRR ALAHHHHHHHHHHHHHH AAAAKKKBARRRRRR

Yasinta Ngonyani said...

Alahandulilai Mwenyezi Mungu awe pamoja nasi Ied njema kwa wooooteee popote pale.

mumyhery said...

Shukran na kwako pia