Tuesday, September 8, 2009

Nawaza...Niwazue.

LABDA MIMI NI MIMI KWA KUWA HAKUNA MIMI ZAIDI YA MIMI
Sijamuuliza mke wangu na sitathubutu kumuliza kwa kuwa "NINAWAZA KWA SAUTI TU". Mawazo yangu yanauliza kuwa, kwa wale wapendano, HIVI NAMPENDA UMPENDAYE KWA KUWA NDIYE BORA KATI YA WABOVU ULIOWAONA AMA KWA KUWA NDIYE BORA KWA AMBAO UMESHAWAONA? (Best among the worst ama Best so far?)
Nauliza kwa sababu najua kile kiitwacho ubora chaweza kubadilika kulingana na mazingira, watu anaokutana nao na hata upeo wa mtu. Na UBORA huu (uwe ni tabia ama muonekano) ni kati ya vitu ambavyo tunajifunza na kuvibadili na kuvithamini kwa namna tofauti kila siku / kila nyakati. Kwani unadhani tunatumia asilimia ngapi ya uwezo wa ubongo wetu? Wataalamu wanasema tunatumia kati ya 0.1%-10% ya uwezo wa ubongo wetu katika maisha yetu (soma HAPA) na ndio maana najiuliza kama ungeweza kuongeza uwezo wa ubongo wako mara kadhaa (tuseme 2) unadhani ungekuwa unamuona mwenzi wako umuonavyo sasa? Labda angekuwa bora zaidi (maana ungeongeza aina nyingine za ubora) na labda ungemuona hakufai (kwani ungeweza kupunguza maana za ubora). Lakini kwani uzuri ni nini na unaonekanaje miongoni mwa macho yetu?
Unadhani kuna mzuri zaidi ya wewe ujinavyo? Pengine hakuna ajuaye uwezo wako katka kutenda na kuwaza yale yasiyoelezeka na ndio maana unashindwa kumfafanulia mwenzako namna alivyo wa muhimu kwako. Na labda ndio sababu mwenzako hajui madhaifu yako na ndio maana mko pamoja.
Lakini unadhani ungekulia katika mazingira mengine na bado ukakutana na huyo uliyenaye ungeendelea kuwa naye?
Je kama ngekuwa unaishi maisha ya kifahari ama kifukara zaidi ya uliyoishi mlipokutana unadhani ungekuwa naye? Na labda mmoja wenu asingempa mwenzake nafasi ya kudhihirisha kile kilichowaunganisha.
Lakini haya hayatibiki jamani Si ndio???????
Ungekuwa tofauti na ulivyo (kama ninavyouliza hapo) yawezekana usingesona hata haya niliyoandika. Lakini nimeandika kwa kuwa "NAWAZA KWA SAUTI"
Siwezi kujielezea nilivyo na kwanini nampenda nimpendaye na kwanini anipendaye ananipenda. Ila najua kuwa MIMI NI MIMI KWA KUWA HAKUNA MIMI ZAIDI YA MIMI
Wewe je?
Tuonane Next Ijayo

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimependa mada hii MIMI NI MIMI KWA KUWA HAKUNA ZAIDI YA MIMI safiiii sana hakuna mwingine kama mimi:-)

Fadhy Mtanga said...

Mimi ni mimi kwa kuwa hakuna zaidi ya mimi.
Nimeipenda. Mkuu shukrani sana kwa kunifikirisha vilivyo.

Faith S Hilary said...

Quoting "MIMI NI MIMI KWA KUWA HAKUNA MIMI ZAIDI YA MIMI". Naona wengine pia they liked it like I did.

Back to what you were talking about...I am "commenting" right?, and say what I "think" right? Ok so here it goes...I believe kwamba no matter where you are right now, I feel like it is suppose to happen kwamba wengine waishi maisha haya na wengine waishe maisha yale (thats my belief).

Let's just say you were suppose to live there, meet the person you met, be with her and spend the rest of your life with her (just saying). Other people (maybe) are suppose to live somewhere else and maybe not meeting anyone and yet life goes on. I feel like "things happen for a reason too". Either it is a bad thing or a good thing. Life goes on. So the thought of "what if..." doesn't really get to me (if I am being honest).

Duh...my longest comment yet...Guiness World Record lol!!! Byee!!!

Mzee wa Changamoto said...
This comment has been removed by the author.
Mzee wa Changamoto said...

Asante Da Yasinta kwa kuipenda mada. Kaka Fadhy nashukuru kuwa nifikiriapo kufikirisha, nafikirishwa na fikra za wafikirishwaji. Da Candy,umesema "So the thought of "what if..." doesn't really get to me (if I am being honest)."
Kwa hiyo tatizo ni wazo la "what if?" ama the way we what ifs???
What if usingeamua kujibu?? Lakini ukaamua kujiuliza what if nikijibu niaminivyo?
Nadhani hapa ni kama nilicyowahi kuandika kuwa "what if we "what ifs" positively?"
Kama uliikosa isome hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/11/what-if-we-what-ifs-positively.html

Faith S Hilary said...

Mmh..nani tena anakuchokoza kaka naona "removed comments" anyway back to what you said...reading your article of "what if" "positively". Hakuna tatizo neither kwenye the what if and it may be how people think of the "what if" (I am getting confused lol). So anyway I am not going to talk the best point ever but the thing is I never use "what if". I haven't asked myself right now "what if I don't answer back, what is gonna happen...is he going to ask me about it". Somehow I never use it.

I said the "what if" mostly on the part kwenye hii post ulivyosema "nge"..."ungekuwa unaishi", "ungekuwa naye", "asingempa". Na ndio maana nikasema the "what if" doesn't work for me because I don't use it. So my conclusion on this is just go with the flow of life. I believe things happen for a reason and they are suppose to happen. Any further questions just holla! :)

Mzee wa Changamoto said...

Hakuna anayechokoza Dada. Hiyo comment imekuwa removed na author mwenyewe. Nadhani alikosea ama ali-log in kwa jina ambalo hakutaka lionekane. UNAJUA AJALI HUTOKEA.
So what if tusingekuwa na "nge" kwenye maisha? Unadhani tungeishi tuishivyo?
Lol

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duh. nimechelewa kufika hapa japo sijui ni kwa kiasi gani macho yatu yanaweza kuwa sahihi. kuna vipofu alioko kwenye ndoa, utasema waliona nini wao?

katika kitabu changu kijacho cha kijana wa kizazi cha dotcom niliandika juu ya wadhungu kuwatamani wembamba wasiokuwa na kushuzi/choo au tako wakati waafrika wakiwatama wanene, wenye kishuzi kirefu na matiti ya kunyonyesha mpaka wanyama.

so ni mazingira na hisia. wote wanavitafutwavyo na wote lengo kuu ni kuzaa hata kama wanadhani wanataka kubusiana, kupapasana na kunyonyona ndimi na kusababisha mvua za misuguano.

ni uamzi zaid wa kuishi pamoja ili kufanya ngono na ujinga mwingine badala ya upendo.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duh. nimechelewa kufika hapa japo sijui ni kwa kiasi gani macho yatu yanaweza kuwa sahihi. kuna vipofu alioko kwenye ndoa, utasema waliona nini wao?

katika kitabu changu kijacho cha kijana wa kizazi cha dotcom niliandika juu ya wadhungu kuwatamani wembamba wasiokuwa na kushuzi/choo au tako wakati waafrika wakiwatama wanene, wenye kishuzi kirefu na matiti ya kunyonyesha mpaka wanyama.

so ni mazingira na hisia. wote wanavitafutwavyo na wote lengo kuu ni kuzaa hata kama wanadhani wanataka kubusiana, kupapasana na kunyonyona ndimi na kusababisha mvua za misuguano.

ni uamzi zaid wa kuishi pamoja ili kufanya ngono na ujinga mwingine badala ya upendo.