Thursday, September 24, 2009

Ni mipasho tangu enzi mpaka sasa. Hivi wanatumwa ama wanaagizwa???

"United Nation should be dealing with equal rights, it is the only chance it can give us INTERNATIONAL PEACE, they only pretend to be what they're not. One day, one day, i know there'll be PEACE. There will be peace on earth" Dwight Bushman Duncan
Nilimsoma Castro na speech yake ya masaa 4 na nusu. Nikamsikiliza Bush alipotoa speech kuhusu Saddam. Nikamsikia Chavez "alipomwaga radhi" mbele ya Umoja huu huu wa mataifa. Kisha Ahmadinejad naye akaweka sera zake. Jana tulikuwa na Ghaddafi akimwaga news bin news.
Napenda kujua kama hawa viongozi huwa wanakwenda "Umojani" na hoja za kitaifa ama pale ni kwenda kunangana wakijua ulimwengu unawaangalia?
Nina hakika kuna namna ya kujiuliza hili kwani japo halijatokea na wala halitegemei kutokea kwa Rais wangu, nimetokea kujiuliza kama Rais kama Kikwete huwa anawajulisha wabunge (ambao wanastahili kuwa wawakilishi wa wananchi) kuwa anaenda Umoja wa Mataifa hivyo akusanye maoni na kujua MAHITAJI NA HOJA HALISI ZA MTANZANIA ama?
Najiuliza tuuuuu, hivi huwa wanatumwa ama wanaagizwa???? Ama wanasema waonavyo wao?
Salamu toka SHAMBA

5 comments:

Koero Mkundi said...

Kaka hakuna jipya..hizo ni kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji,,,watasema lakini haki haitapatikana, kwani mataifa makubwa hutumia umoja huo kujinufaisha kimaslahi huku nchi nyingine zikitumiwa kufanikisha malengo yao

Yasinta Ngonyani said...

Mara nyingi pia huwa nimekuwa najiuliza kama hawa maraisi wayasemayo yanatoka kichwani mwao au kuna mtu mwingine anasema na yeye anatoa maagizo tu.Na sijui kama wanaelewa wana sema nini.

Mzee wa Taratibu said...

Lakini Koero hawa watatu ni kiboko ya America, Ahemd Nijad, Ghadhafi na Chavezi wanasema kweli hawajali wala kuogopa mtu pale si kama wengine, wanakwenda pale ni picha na kusinzia.

Simon Kitururu said...

Eti umoja wa MATAIFA wakati sye Tanzania hata umoja wa Taifa hatuna na kama upo nyufa kibao!:-(

John Mwaipopo said...

Mie nadhani tunawatuma kutusemea ingawaje wanasema ya kwao. kibali cha kutumwa nasi wanakipata kila baada ya miaka mitano. huwa tunawapa kibali hiki kwa kuwa wamejinadi kwetu kuwa wao ni majiniasi, hivyo tuwape tu. hapan' shaka wanatuwakilisha.