Sitaki kuingia katika kusaka chanzo cha tukio hili, lakini hakuna ubishi kuwa kukosekana kwa HAKI NA USAWA KWA WOTE kumekuwa tatizo kubwa katika yale yaendeleayo sasa. Haijalishi nia ya watendaji ilikuwa nini, ila kushindwa kusaka walio kiini cha matatizo yao na kuua wasio na hatia ndio chanzo cha malipizo tunayoyaona yakiendelea sasa hivi. Marekani iliamua kwenda kuwasaka waliohusika na katika kusaka huko inaendelea kujikuta ikisababisha vifo kwa wasiohusika. Vifo hivyo vinazidi kujenga chuki na nia ya visasi na tunaona kuwa jinsi vita inavyoendelea ndivyo visasi vinavyoongezeka. Yaani ni kama tunaongeza akiba ya visasi baina yetu kwenye akaunti ya chuki tuliyojifungulia. Luciano aliimba akisema "we kill the wicked but still more rise, without proper justice we shouldn't be suprised." Ina maana kuwa waliosababisha haya yaliyotokea Sept 11 walikuwa wakilipiza kisasi kwa wanayoamini wanastahili lakini wakayatenda kwa watu wasio na hatia. Na hili ndilo tatizo la kutokuwa na HAKI NA USAWA.
Leo hii tunaye Winston Hubert McIntosh ama Peter Tosh ambaye naye aliuliwa na aliyekuwa rafiki yake Dennis 'Leppo' Lobban tarehe kama ya leo lakini miaka 22 iliyopita ( Sept 11 1987) Tosh aliwahi kuimba kuhusu tatizo la haki na usawa katika wimbo wake wa EQUAL RIGHTS na alilieleza kama chanzo cha matatizo mengi makubwa kwa kuwa watu wengi hawataki kutafuta suluhisho la matatizo na kujikuta wanakwepa na "kuendeleza" tatizo. Mfano ni watu kujifanya wakitafuta amani huku wakipuuzia haki na usawa na wengine kutamani kwenda mbinguni lakini hawataki kufa. Mmmmmmmhhh!!!!!!Msikilize huku ukisoma mashairi yake na kumtafakari
Everyone is crying out for peace yes
None is crying out for justice
(2x)
(CHORUS)
I don't want no peace
I need EQUAL RIGHTS AND JUSTICE (3x)
Got to get it
Equal rights and justice
Everybody want to go to heaven
But nobody want to die
Everybody want to go to up to heaven
But none o them (2x) want to die
CHORUS
(Just give me my share)
What is due to Caesar
You better give it on to Caesar
And what belong to I and I
You better (2x) give it up to I
CHORUS
(I'm fighting for it)
Everyone heading for the top
But tell me how far is it from the bottom
Nobody knows but
Everybody fighting to reach the top
How far is it from the bottom
CHORUS
Everyone is talking about crime
Tell me who are the criminals
I said everybody's talking about crime, crime
Tell me who, who are the criminals
I really don't see them
CHORUS
There be no crime
Equal rights and justice (Precedes each line below)
There be no criminals
Everyone is fighting for
Palestine is fighting for
Down in Angola
Down in Botswana
Down in Zimbabwe
Down in Rhodesia
Right here in Jamaica
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
2 comments:
"Marekani iliamua kwenda kuwasaka waliohusika na katika kusaka huko inaendelea kujikuta ikisababisha vifo kwa wasiohusika. Vifo hivyo vinazidi kujenga chuki na nia ya visasi na tunaona kuwa jinsi vita inavyoendelea ndivyo visasi vinavyoongezeka. Yaani ni kama tunaongeza akiba ya visasi baina yetu kwenye akaunti ya chuki tuliyojifungulia"
Sina la kuongezea kwani umeieleza hii "vicious cycle" ya chuki, visasi na maangamizi vizuri sana!
inasemekana hili ni tambiko la wa freemasons. chukua namba hizo, 9+1+1=12.
kwa mnaojua unajimu namba 12 ina maana kuuubwa.
anyway, tuamini ni waisilamu wanaichukia marekani
Post a Comment