Tuesday, October 20, 2009

Kuna mengi ya kumkumbuka Baba wa Taifa....Mhe Waziri Asha A. Juma

Mhe Waziri na waandaaji wa sherehe hiyo Mr & Mrs Tingling
Mhe Waziri na baadhi ya wageni waalikwa
Watanzania wamekumbushwa kuwa kuna mambo mengi ya kukumbuka na kutekeleza kila tumkumbukapo Baba wa Taifa Mwl Julius K. Nyerere. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Kazi, Vijana na Maendeleo ya Wanawake na Watoto Mhe Asha A. Juma alipopata muda mfupi wa kuongea na blogu hii baada ya kumalizika kwa sherehe za kumkumbuka Hayati Baba wa Taifa zilizoandaliwa na Nyerere Health and Education Fund na kufanyika jijini Washington DC.
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa sherehe hizi kufanyika ambapo mwaka jana zilizambatana na maelezo toka kwa wajukuu wa Hayati Mwalimu na wengine waliohudhurua na waweza kutazama habari na picha zake kwa kuBOFYA HAPA

Sehemu fupi ya mahojiano yetu.......

4 comments:

chib said...

Hapa Rwanda, jumapili iliyopita kulikuwa na ibada maalumu ya kumkumbuka Nyerere iliyoandaliwa na wanyarwanda waliowahi kuishi Tanzania.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

huyu jamaa alikuwa binadamu wa aina yake na ni binadamu tunayemuhitji kwa wakati huu kuliko wakati mwingineo wowote

viva afrika said...

vema na haki kama tutamuenzi kwa kuyafuata mema alotuagiza, alikua ni mwafrika halisi aliyeweka mbele maslahi ya afrika. ama baada ya hayo kaka mubelwa kuna ujumbe wako kwenye baraza langu, fanya kutembelea.
JAH bless

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Yote mliyosema ni kweli. Ndiyo maana nilishangaa sana Dada Subi (nukta77) na mimi tulipoambiwa kuziondoa video zake mara moja kwa sababu ambazo hazieleweki. Ndiyo maana niliamua kulalamika katika makala ya "Mwalimu Nyerere na Jangwa la Kiitikadi" iliyochapishwa katika gazeti la Kwanza Jamii la wiki hii (ipo pia katika blogu yangu). Profesa Mbele aliongezea kwa kusema kwamba mpaka leo hii ukitaka vitabu vya Nyerere (hasa kile cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania) ni afadhali ujaribu Kenya lakini Tanzania huwezi kukipata. Kuna watu ambao (kwa sababu zisizoeleweka - pengine ni mafisadi) hawataki mawazo ya Mwalimu yaendelee kuenea miongoni mwa Watanzania. Inashangaza sana!