Saturday, October 17, 2009

Ulimwengu utembeao baharini

Picha toka www.goodnewsfinland.com
Baada ya miaka 5 ya kazi ngumu ya kubuni, kupanga na kujenga, hatimaye kampuni maarufu ya usafirishaji ya Royal Carribean inataraji kuiweka baharini meli yake kubwa na ya kisasa zaidi na ambayo ndiyo meli aghali kuliko zote.
Ikiwa na urefu wa futi 1,184 na wafanyakazi wapatao 2,160, meli hiyo itakayojulikana kama OASIS na yenye thamani ya dola Bilioni 1.4, itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 5,800 iwapo kila chumba kitachukua abiria wawili
na ndani mwake (hasa sehemu ya kati inayoitwa Central Park) kunategemewa kuwa na miti na mimea ipatayo 12,000.
Gharama za tiketi yake zakadiriwa kuwa dola 1000 kwa siku saba kwa mtu mmoja zinazoifanya kuwa aghali zaidi hasa ukizingatia kuwa meli nyingine za kampuni hiyohiyo zaanzia gharama ya dola 490 kwa siku saba
Binafsi najihisi uzito kusafiri humu. Nadhani hata siku saba hazitoshi kumaliza kuizungukia.
Hebu iangalie hapa inavyooneshwa

10 comments:

Anonymous said...

baada ya titanike ndo hii inafwata? haya, watuhadithie watakao kwenda huko

Mzee wa Taratibu said...

Sisi yetu macho tu.

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli sie yetu macho

Fadhy Mtanga said...

Kwanini yawe yetu macho? Suala ni kuiwekea mikakati na angalau 1% ya kakipato ili Mungu akikupa uzima uje kuiona. Hata kama itachukua miaka kumi, bora uzima na afya njema.

Faith S Hilary said...

Kaka, niazime $1000 nitakurudishia...unless its my Halloween gift

Mzee wa Changamoto said...

Da Subi, nahisi "my heart will go on" nikiingia humu. Mzee wa Taratibu na tutazame (kwa kupenda ama kuto-afford) maana hiyo ina mazuri mengi na hatari nyingi pia. Da Y!! Na tuwatumbulie. Kaka Fadhy nimekupata na nashukuru kwa kubarizi. Da Mdogo F, njoo uchukue na usirudishe, ila nauli toka ulipo mpaka hapa ni $1000.99 sasa sijui hesabu itakuwaje hapo?
Lol
Blessings to y'all

Albert Kissima said...

Sijapanda hata boti! Sasa huu ulimwengu wa baharini,sijui inakuwaje, ka!

John Mwaipopo said...

au ndio watapanda wateule watakaoiona mbingu. really nice.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kesho kutwa tu nitapanda meli maarufu kama mv victoria kuelekea mwanza na kwa hiyo nina uzoefu naweza semma usafiri wa majini ni bomba il kwa hawa DUH

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kesho kutwa tu nitapanda meli maarufu kama mv victoria kuelekea mwanza na kwa hiyo nina uzoefu naweza semma usafiri wa majini ni bomba il kwa hawa DUH