Wednesday, October 28, 2009

Mkaribishe Dada Agnes Anderson wa "kiduchu"

Niliwahi kusema kuwa kama tutapanga kutafuta makao makuu ya Blog nchini Tanzania, basi yawe nyanda za juu kusini. Yaani huko kuna kila kitu, lakini kila kitu kwa mTanzania. Kuanzia kwa Mwenyekiti Mjengwa mpaka Kaka Msangi, Kwa Kaka Fadhy na hata mzee wa Matukio Daima Kaka Francis Godwin, Mzee wa Viva Afrika na hata Kakangu sana Shaban Kondo. Kuna Anga za michezo na hata Mtu mzima Allen Phillips. Siwezi wataja wote kwani ni kama vile nyanda hizo ni KITOVU CHA BLOGU ZA WATANZANIA KWA WATANZANIA.
Ninalomaanisha hapa ni kuwa asilimia kubwa ya wandugu hawa, wanaandika kuhusu nchi na jamii yetu.
Wanatujuvya mengiyaendeleayo na binafsi ninaweza kuwa nyumbani kimawazo niwapo nao.
ASANTENI SAAANA.
Lakini uhitaji ni mkubwa wa habari na uchambuzi. Wenye kuleta taswira na wenye maandishi mengi. Wenye muzii na burudani na wenye JAMII kwa ujumla. Kila mtu ana mengi mema na kila mtu ana yake mema. Na ni katika kututimizia hili, nakutana na huyuuuu mdada mwenye staili ya "kiasi". Hataki kukupa mengi bali kwa kiasi kikutoshacho. Anakupa KIDUCHU
Anapolizungumzia "jamvi" lake anasema "
utapata mitindo kiduchu,muziki kiduchu,urembo kiduchu nk...lakini kiduchu ya hapa itakutosha."
Basi tuombe nini zaidi ya kitutoshacho????
Si tumeshaonywa TUWE NA KIASI? Na sasa twaambiwa kuwa "kiduchu" ya ndani ya KIDUCHU BLOG itatutosha. Mtembelee kwa kubofya hapa

Karibu saaana Da Aggie na ukipata muda kiduchu usisite kupita hapa na kwenye blogu nyingine nyingi zifikirishazo watu kiduchu na ukipita acha maoni kiduchu kwa CHANGAMOTO kiduchu zisemwazo kiduchu kwa kuwa twasemea kiduchu walio na uwezo kiduchu wa kiwaona wale walio na idadi kiduchu lakini wana mengi na kututawala na kutufanya tusiongezewe katika kile kiduchu tupatacho.
Najua umeanza (kama tulivyo sisi) na kwa pamoja tutaweza kusonga.
Nikukaribishe ktk safari hii MUHIMU NA IWEZEKANAYO kwa kibao chake Bob Marley akisema KEEP ON MOVING......
Karibu Dada Agnes

1 comment:

AGNESS ANDERSON said...

ahsante mno kaka, umezidi kunipa moto kusema ukweli...nakuahidi kufanyia kazi yale yooote ambayo umenihusia na kutekeleza hayoyote nliyo yaahidi na mengine zaidi japo kwa uduuuchu lakini mwisho wa siku tunakuwa tumeelewana... thanx much aisee.