Wednesday, October 28, 2009

U-wapi Da Digna Abraham? Popote ulipo, uwe salama

Dada Digna, ni miezi sita na siku kumi na moja zimepita tangu uweke post kwenye baraza lako. Twatumai na kuomba kuwa popote ulipo UKO SALAMA na kwa kila jema utendalo, unatuandalia mafunzo mengi mema ya kutufanya tu-Behave free.

Kwa wanajamvi wenzangu, tukumbuke kuwa blog yake hiyo njema inajieleza (na hapa nanukuu) "Behavefree ni blog itakayokuwa inajadili tabia mbali mbali za vijana ikiwa ni moja ya changamoto zinazowakabili vijana katika kufikia malengo yao ya baadaye katika jamii. Kutokana na changamoto hizo wamewezaje kubadili tabia zao na kufikia malengo yao na hatimaye kupata mafanikio katika kuendesha maisha yao. Pia kutakuwa na habari za kuchangamsha, kufurahisha na kuelimisha."
Kwa hakika hatutaki kuyakosa yote haya kwani ni MUHIMU katika maisha yetu

Japo hajakuwepo kwa muda, lakini waweza angalia HAZINA aliyoiacha kwa mara kadhaa alizokuwepo kwa kutembelea blog yake ya Behavefree (bofya hapa)

Wana Changamoto twakuombea urejeo mwema na mafanikio katika yote MEMA ufanyayo.


Blessings

No comments: