Tuesday, November 17, 2009

Heri ya siku ya kuzaliwa Mama Mzazi

Mama na Baba
Miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nawasiliana na Dadangu Zena Chande, na katika kuzungumza kuhusu maisha na uzazi akaniambia kuwa "niliyopitia wakati wa ujauzito wa mwanangu yamenifanya nimthamini zaidi Mamangu. Kwa bahati mbaya ameshatangulia mbele ya haki." Nilimsikia, nilimuelewa na tuliendelea na maongezi mengine mengi. Nami wakati wangu ukawa unakuja. Wakati wa Maisha ya maandalizi na uzazi. Ndipo nilipomuelewa zaidi. Na nikafarijika kuwa amempenda zaidi mzazi wake ambaye alionesha upendo kwake kiasi cha kumfanya asijue yale ambayo alipitia wakati wa kumlea yeye hasa enzi za utoto.
Ni faraja kuwa Dadangu huyu (kama tulivyo wengine wengi) tunakuja kuutambua mhangaiko wanaokuwa nao wale watukuzao baada ya kuwa tumepitia yale tudhaniayo kuwa ya kipekee kwetu. Lakini tunakuja kutambua na kuwaheshimu, na wawepo ama wasiwepo, bado (kama wanatuona) wanajivunia kuwa ule UELEWA WA UTHAMINI waliowekeza kwetu unafanya kazi (hata kama ni "too late")
Wiki chache zilizopita nilikuwa nazungumza na Babangu, nikamweleza ninavyokesha kumlinda "mheshimiwa" Paulina (sijui kama nilitegemea anionee huruma ama la). Nikasikia kitu kama tabasamu kutoka kwake kisha kilichofuata ni taarifa kuwa "HATA NA WEWE ULIKUWA HIVYOHIVYO"
Duh!!! Nilidhani nilikuwa napendwa kwa kuwa sikuwasumbua. Kumbe nilipendwa kwa kuwa WAZAZI WETU WALIKUWA NA WANA UPENDO NASI LICHA YA KELELE, MIKESHA, MIHANGAIKO NA NJIA ZOOOTE NGUMU TULIZOWAPITISHA.
Nilinywea kujua kuwa nilisumbua kuliko mwanangu na kama alivyosema Dada Zena, hilo likanifanya niwathamini zaidi na zaidi wazazi wangu. Sio tu kwa kuwa walinihudumia hata pale nilipokuwa nawasumbua, bali pia kwa kuwa hawakuhesabu niliyowatendea na hata hawakunisimulia ili niwapende zaidi.
Kwangu mimi wazazi wetu ni zaidi ya mashujaa katika maisha yetu
..Kwanza walikuwa na wameendelea kuwa sehemu kubwa ya familia zao na hiyo ilitufanya sisi kuunganika na familia zao na kuendelea kujua umuhimu wa kuwa nao licha ya kuwa maisha yetu ya awali tuliyatumia mbali na asili yao.
..Wakaendelea kujenga u-familia (japo laonekana kuwa jambo dogo, lakini familia nyingi leo hii zimemomonyoka) ambao umetuwezesha kuishi vema na wanandugu hasa pale tulipoondoka mikononi mwao. Maisha yetu kwa Baba na Mama wadogo an wakubwa, Wajomba na Mashangazi na ndugu zao wengine ni kama tuko nyumbani na ni kwa kuwa wote (wazazi wetu na ndugu zao) wameendeleza u-familia mpaka kwetu
..Wamejenga uhusiano wa kirafiki na watu walio na mitazamo chanya ya maisha kama wao na hivyo kutuunganisha na watu ambao mpaka leo kuwa nao ni sawa kuwa na wazazi
.. Wakatujenga na kutukuza katika makuzi ya Imani na Adabu ambayo kwa hakika yametufanya kuendelea kuwa na NDUGU mahala pote tuendapo hivyo kuturahisishia maisha.
.. Wametufunza KUHESHIMU watu na utu na kukubali kutokukubaliana kwa Heshima pale inapostahili.
Haya ni machache kati ya mengi ambayo wazazi wetu wameonesha kwetu na leo hii twaikumbuka siku ya kuzaliwa ya mmoja wao. MAMA YETU MZAZI.

Narejea kuandika yale niliyoandika mwaka jana siku kama ya leo kuhusu Mama zetu kuwa
" We each get just one MOTHER to love a lifetime through, One MOTHER to encourage us in everything we do. But one MOTHER is so many People blended into one. A source of inspiration and happiness and fun. A MOTHER hears out every word. She listens with her heart, shares and always cares, thinks of others first and she'll love us just like always even when we're at our worst. She brings such happiness with kindness she gives and creates a GOOD EXAMPLE simply with the life she lives. YES! We only have ONE MOTHER to look up to and to praise and NO ONE ELSE IN ALL THE WORLD can MATCH HER LOVING WAYS"


HERI YA SIKU YA KUZALIWA MAMA YETU.
Wewe ni SHUJAA wa maisha yetu na wale wote tuhusianao nao na kwa hakika TUNAJIVUNIA wewe kuwa MAMA yetu. Tunakupenda na kukuthamini na tunakutakia kila la kheri katika kukumbuka siku yako ya kuzaliwa na pia katika miaka ijayo yenye afya na nguvu tele

5 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ngoja mimi nianze: Happy Birthday Mama Changamoto! Hongera kwa kutuletea shujaa, mpigania haki na mwelimishaji mkuu wa jamii. Kazi nzuri uliyoifanya tunaiona. HONGERA SANA!!!

NB: Unafanana kweli na Baba Changamoto!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ukielezea uzuri wa wazazi na furaha ya kuwa na wazazi wengine hatukuelewi. niliishi bugandika bukoba huku baba akiishi Nairobi - Kenya. nilikutananaye baadaye lakini si muda mrefu akaacha mwili wake (kufa?)

nilimwona mama kwa mara ya kwanza mwaka 2001, uhusiano wa mama na mtoto nilioulilia mpaka leo haujawahi kuwepo.

mengi ya malezi yangu yalinifanya nishangae dunia ya walezi / wazazi

just imargini nina mama, and I love her but.......

najivunia kujitambua vinginevyo post kama hizi zingeweza kunifanya nilie siku nzima, but life goes on./

anywa, HAPPY BIRTHDAY mama changamoto na yawezekana uamzi wa kumleta duniani ulikuwa sio uamzi bali ilibidi na hivyo ukawa uamzi wa mambo mengine na ghafra ndo changamoto zenyewe

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa siku ya kuzaliwa mama. Kwa mimi mama ya rafiki yangu basi ni mama yangu pia nadhani Mzee wa Changamoto hutajjali kumwita mama.
Ni kweli umefanana sana na baba "Changamoto"

PASSION4FASHION.TZ said...

HAPPY BIRTHDAY MAMA.

Mama weee!!kumbe mzee wa changamoto ni photocopy ya baba? yaani hata mtu hawezi kuuliza,mmefanana mno!hongera sana.

Faith S Hilary said...

Passion4fashion na Masangu wamenisaidia maana I was trying to work out umefanana na nani zaidi (just for fun) lol anyway I got nothing much to say other than HAPPY BIRTHDAY MAMA!!!