Thursday, November 26, 2009

Kutoka Bloguni!!!! Twende majaridani na magazetini

Kakangu Albert wa blogu ya MWANGAZA aliwahi kuuliza kuhusu itakavyokuwa kama makala nono ziandikwazo kwenye blogu zetu zingeweza kufika kwenye magazeti. Tukawa tunawafikia kina Bibi yangu kule Bushasha na wengine mikoani. Lakini si jambo geni kwani tuliwahi kulijadili siku ileeeee ambayo Da Koero aliandika kuhusu Yasinta. Na binafsi nikachukua hatua moja mbele na kumwambikia mhusika wa Gazeti tuliloona lina nafasi kubwa ya kutuunga mkono kwani ni la mwana-blog na lina wana-blog wengi la KWANZA JAMII kuhusu hili.
Na leo nilipofungua hapa kwa Da Koero na kukuta anahamasika kusogea gazetini nikajumiisha na maandishi haya ya Kaka Matondo nikaona ni vema kukumbushana kuwa kutakuwa na manufaa na itawafaa JAMII ambayo tunahangaika kuielimisha na kuikomboa.
Barua yangu kwa KWANZA JAMII ilisema


Kutoka bloguni
Saturday, April 18, 2009 3:24 PM
From:
"Mubelwa T. Bandio"
View contact details
To:
habari@kwanzajamii.com
Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
Natumai kuwa mu-wazima na mnaendelea vema na harakati za kuikomboa jamii. Kwanza niwapongeze kwa ujio wa gazeti jipya lenye uelimishaji. Gazeti lenye mchanganyiko wa chambuzi na kuonekana kuwa na mtazamo wa kuinusuru jamii.
Pia katika nililogundua ni kuwa gazeti hili lina timu ambayo wengi wao pia ni waandishi wa blogu mbalimbali za ki-chambuzi. Kwangu ni nyota njema kuwa waandishi wa blogu wana nafasi nzuri ya kuweza kusogeza habari kutoka kwenye mfumo huu kwenda kwenye uchapishaji (japo wengine ndiko walikoanzia). Lakini nakumbuka kuwa wiki chache zilizopita mmoja wa wana-blog (Dada Koero Mkundi wa www.koeromkundi.blogspot.com ) aliandika habari kumhusu binyi mmoja aitwaye Yasinta ( http://koeromkundi.blogspot.com/2009/03/kutana-na-yasinta-mjasiriamali.html) ambayo iliwagusa wasomaji wengi na kukawepo na maoni ya namna ya kuwezesha kufikisha habari kama hizo "nje ya blogs" na kuna waliosema wangekunadikia kuomba ufikirie hili. Sina haika kama walifanya hivyo, bali nami nimeona niandike kuona kama unaweza kufikiria kuwa na "kona" ya kutoka bloguni ambayo kwa kutumia waandishi wa blog wanaoandika kwenye Kwanza jamii mkaweza kuchagua habari kutoka blog mbalimbali mnazohisi zinaifaa jamii yetu.
Ni hayo tu na naamini utayafikiria.
Blessings

4 comments:

Bennet said...

Ni kweli makala nyingi kwenye blog zetu ni za kuelimisha jamii iwe mijini au vijijini. Hongereni ambao mmeweza kuwafikia wasomaji zaidi kwa njia ya makala za magazetini

Albert Kissima said...

Nashukuru kaka kwa kuendelea kulitilia mkazo swala hili.Tusikate tamaa, tusivunjike moyo,naamini ipo siku sauti na harakati za wanablog sitasikika na kusomeka na hata wale wasio na uelewa wa intaneti na walio vijijini na sehemu nyingine ambazo kwa namna moja ama nyingine wanashindwa kuyapata ya bloguni kirahisi hususani kupitia kwenye intaneti.

Fadhy Mtanga said...

Ni changamoto nzuri. Nami napaswa kuyasogeza mashairi kule.

徵信社 said...

I love it! Very creative!That's actually really cool.
謝謝你的文章分享,請你有空到我

參觀,Thanks!:))))