Thursday, November 5, 2009

Miaka 6 baada ya kifo chake, mmoja kabla a UCHAGUZI MKUU

Ujumbe wake ni muhimu zaidi kwa jamii hivi sasa. Picha toka www.kibirafilms.com
Katika kuelekea UCHAGUZI MKUU UJAO (2010), nimeona ni vema kuangalia nyuma kukumbushana YALE YALIYOFICHWA NA KUPUUZWA NA JAMII LICHA YA KUELEZWA BAYANA NA WASANII WETU.
Mpaka alipofariki August 12, 2003, Justine Kalikawe alikuwa ndiye msanii mwenye albamu nyingi zaidi za Reggae nchini Tanzania (8 za audio na 3 za video katika miaka 16 aliyodumu katika muziki wa Reggae). Aliimba katika mchanganyiko wa Kiswahili, Kihaya na kwa lugha itumikayo Uganda na alikuwa mtetezi mkuu wa jamii na hasa jamii ya wanyonge. Aliongelea kuhusu matezo yao, pilika zao, sababu za wao kukimbia wanakozaliwa na hata namna ambavyo JAMII inaweza kuwa msaada kwa vijana hawa.
Na leo ninaanza na mkusanyiko wa nyimbo alizoimba ambazo ziliunganishwa katika wimbo wa kumuenzi ulioimbwa na mkusanyiko wa wasanii nyota Tanzania waliojiita TANZANIA REGGAE FAMILY. Wimbo uliitwa HAKUNA na sehemu kubwa ya mashairi yake yaliazimwa moja kwa moja toka ktk nyimbo zake.
Ukiusikia mwanzo, Justine anawakumbusha walimwengu kuwa "hakuna atakayekuja kukufanyia yale utakayo yafanyake, hakuna atakayekuja kukuletea, yale utakayo uyapate."
Na haya ndiyo tunayostahili kuwaelimisha wananchi wetu sasa hivi nyumbani kuwa TUSITEGEMEE WAGOMBEA MBALIMBALI KUTULETEA MABADILIKO NA MAENDELEO TUTAKAYO. Yatubidi tuyasake wenyewe.
Pia Justine "aliomba kuishi kwa amani, Mungu amwepushe na majanga. Ya Walimwengu si madogo." Hakuna anayeweza kupuuza nguvu ya SALA kuepukana na "ubaya" wa walimwengu. Ni muhimu na yatupasa kulizingatia hili.
Lakini pia Justine amekuwa akiimba "kuhusu chanzo cha tatizo kuwa ndilo tatizo" na aliamini kuwa hilo ndio chimbuko linalopuuzwa na wengi. Tunaona namna ambavyo aliweza kuona yale yanayoanza kuimung'unya nchi yetu alipowahi kuonya kuwa "utaratibu na ukimya wetu visituangamize sisi wenyewe. DINI, SIASA, PESA na UKABILA visituvuruge. Ni muhimu sote tukizingatia wajibu wetu". Lakini pia tunaona anavyowausia viongozi / watawala kuhusu vijana anaposema "Vijawa kupewa vitendea kazi, nafasi ya ushupavu michezoni, KUTOTOFAUTISHA MAISHA YA VIJIJINI NA MIJINI". Na kwa hakika hili linaweza kuwa suluhisho la kupunguza mrundikano wa vijana mijini.
Ni Justine Kalikawe ambaye alifanya vema na kwa umakini kabisa kazi yake ya KULENIMISHA, KUBURUDISHA na KUIKOMBOA JAMII TOKA UTUMWA WA KIAKILI.
Na leo ni miaka 6 na miezi kadhaa tangu afariki, na ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ujao, lakini UJUMBE wake ni HAI leo kama aulivyokuwa wakati akiandika nyimbo zake.
Furahia wimbo huu uitwao HAKUNA

BLESSINGS
Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

6 comments:

John Mwaipopo said...

aaah! mzee wa changamoto you made my day. nilimzimikiaga sana hayati kalikawe. ndani ya kalikawe mtu uliweza kuona ukweli. namaanisha kwa kumtazama tu kwa macho yako mwenyewe mtu uliweza kukiona kuwa alichokiimba hakikutokea mdomoni. mdomo ulikuwa chombo tu cha kuwasilisha ujumbe. maneno ya kalikawe yalitoka rohoni kwake. tofauti na wanamuziki wengine maneno yao yanatoka kwenye lips tu huku macho yao yakikodolea wallet yako uwatunze ama ununue kazi zao walizoimba upuuuzi tu.lo! miaka inakimbia ati. eti leo miaka sita.

kingine justin alikuwa muhalisia. alikuwa akipenda kuishi bukoba kuliko dar es salaam. da es salaam alikwenda kimuziki tu, kurekodi ama kufanya maonyesho. kisha huyooo bukoba. alipenda kulima pia (nadhani ndizi). hata mauti yalimkuta bukoba, pengine angekuwa dar es salaam angepata matibabu (siyakumbuki maradhi yaliyopelekea mauti yake)

mwishoni mwa mwaka 1996 na mwanzoni mwa mwaka 1997 kila kona kule mbeya kulikuwa kukisikia albamu yake (siijui jina kamili) iliyokuwa na songi kama mv bukoba. rafiki yangu siku moja aliniuliuza hivi ni kwa nini nilikuwa na hisia zilezile kama za bob marley nilipokuwa naigiliza nyimbo za kalikawe. nikamwambia zina ujumbe uleule. leo nakumbuka mistari hii

'utaratibu wetu wenyewe unatukandamiza sisi wenyewe, yeyee, yeyee yeahhjhhh"

RIP Justin Kalikawe

chib said...

Umenikumbusha mtu muhimu sana katika muziki wa reggae Tanzania. Mimi nilikuwa kati ya watu wa mwanzo kununua mziki wake, tena kutoka kwake mwenyewe wakati alipopita kwenye kijiwe chetu akiwa na boksi la audio tapes, ziliisha kwa fumba fumbua, hata yeye mwenyewe alishangaa maana hakuwa analeta kuziuza,bali alipitia kwa mshikaji wake kumpa HI ambaye tulikuwa naye hapo

Yasinta Ngonyani said...

Ustarehe kwa amani amina. Naamini mziki wako utaendelezwa kwa hiyo utakuwa nasi daima.

Simon Kitururu said...

Asante sana kwa kutukumbusha mtu huyu Mkuu!

Ni kweli kabisa ujumbe wake uko hai!

Mdoti com-kom said...

Asante! Umenipa mwanga sana kwa kuwa umetumia maneno ya msanii niliyemkubali sana. Ukweli ni kuwa wapo wasanii weng wa muziki wanaotoa jumbe nzuri sana nadhani tatizo lilopo ni maana mpya ya neno msanii, hi imefanya weng wadharau mara tu wasikiapo neno msanii. Lakini hiki kitendo cha wasani wetu kuimba hadith za mapenz 2 ndiko kunakofanya hata wale wenye ujumbe wa maana waonekane ni hao hao. Kalikawe ni wa kukumbukwa. Mungu amlaze mahali pema peponi

mdoti Com-kom said...

Nimejaribu kutafuta cd za kalikawe but am sad kwa kuwa sikuzipata. Please naweza kupata wapi?