Sunday, November 29, 2009

Mtagwa kurejea ulingoni Jan 23 kuwania mkanda wa WBA.

Image courtesy of http://www.phillyboxinghistory.com/
Baada ya kupoteza pambano lake kiutatanishi Oktoba 10 dhidi ya Juan Lopez na kukataliwa pambano la marejeano licha ya kuonesha uwezekano mkubwa wa "kumuumbua" Lopez, bondia mTanzania aishiye Philadelphia Rogers "The Tiger" Mtagwa atapanda ulingoni Jan 23, 2010 kupambana na bondia anayefanya vema saana na nyota ing'aayo toka Cuba Yuriorkis Gamboa.
Pambano hilo litakalopiganiwa New York na kuonekana kupitia HBO, litakuwa ni la kuwania mkanda wa Gamboa wa uzito wa Unyoya (featherweight) unaotambuliwa na Chama cha Ndondi Ulimwenguni (WBA). Usiku huohuo na katika ukumbi huohuo, Juan Manuel Lopez ambaye alipata ushindi dhidi ya Mtagwa atapambana na Steven Luevano kuwania mkanda wa Shirikisho la Ndondi Ulimwenguni (WBO) unaoshikiliwa na Luevano.
Iwapo Mtagwa atavuka kigingi hiki kigumu (kulingana na ubora na upiganaji wa Bwana mdogo Gamboa) atakuwa amejiweka katika mazingira mazuri ya kurejea ulingoni na Lopez kama wataweza kuafkiana katika kuunganisha mikanda kwani yote ni ya uzito mmoja.
Hapa chini ni Video ya pambano la Mtagwa la mwezi uliopita

Kila la kheri katika maandalizi yako Kaka Mtagwa.

10 comments:

sunday simba said...

Tunamtakia kila la kheri Rodgers Mtagwa maana huyu Gamboa ana spidi sana na makonde yake yanalenga sawa sawa itabidi afanye kazi ya ziada kuwa makini na makonde yake. Itabidi aangalie pambano la Jimenez Darling ingawa alishindwa kwenye pambano hilo lakini ni mtu aliyefanikiwa kumwangusha Gamboa baada ya kwenda nae sambamba kwa muda mrefu. Naamini litakuwa pambano la aina yake.

Simon Kitururu said...

Mmmmhh!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

huwa sielewi vitu vingine kama mtu kupigana na mwingine harafu wengine mnashangilia, may b am not normal!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

KILA LA KHERI MTAGWA

Albert Kissima said...

nami namtakia kijana huyu kila la heri,

Mzee wa Changamoto said...

Ni kweli Kaka Triple S. Gamboa ni mashine nzuri na ana advantage ya umri na nguvu.
Kitururu. Usijali ni sehemu ya maisha.
Kamala uko normal wala usijali. Ni kwamba UMEAMUA KUJISAHAULISHA KUWA HAKUNA KITU KINACHOTENDEKA ULIMWENGUNI KIKAPATA SUPPORT YA WOTE.
Ukiweza kukumbuka unikumbushe tafadhali. Lakini najua HAKUNA kinachoshangiliwa na wote. Hivyo na wewe kutoshangilia hili ni UAMUZI tuuu.
Kwa kaka Edo na Albert. Nuff Respect to y'all.
Blessings

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Katika gazeti la "The Ring - the Bible of Boxing" toleo la sasa (January 2010) ukurasa wa 87 Roger Mtagwa ametajwa kuwa ni bondia wa 100 kwa ubora duniani kutokana na alivyomchachafya Manuel Lopez katika shindano lake la mwisho. Ni mara yake ya kwanza kujumuishwa katika viwango hivi vya kimataifa na kwa hili anastahili kuhongereshwa.

Kutokana na kufanya vizuri katika pambano lake la mwisho (japo alishindwa) wachambuzi wanasema kwamba pengine itamwia vigumu kupata wapinzani wazuri wa kupambana naye kwani mapromota wataogopa kuwapambanisha mabondia wao naye wakiogopa kwamba mabondia wao watapigwa. Kwa Gamboa hata hivyo anayo kazi pevu kwani huyo mzamiaji wa kutoka Cuba si mchezo.

Swali langu kwa Kamala: Ni mchezo gani ambao unaushabikia/unaupenda? Kwa nini?

Yasinta Ngonyani said...

Nami pia nmtakia kila la kheri kaka Mtagwa

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

matondo swali lako lina akili sana na labda nifikirie kabla ya kulijibu.

sijui kamanapenda soka maanake siliangaliagi kwa kisingizio kuwa lilnapoteza muda mwingi na hivyo huwa naagalia mechi chache za kombe la dunia! labda napenda volleyball kwa sababu mimi nimchezaji wa volleybal. labda napenda kuogelea kwa sababu pia huwa naogelea lakini katika michezo hiiyo siwajui mastaa wala nini yani na nipale ninapobahatika kuicheza michezo yenyewe.

lakini michezo ninayoipenda (kama kweli naipenda) basi ni vichekesho. nawapenda wachekeshaji wa aina mbali mbali na sipendi kukosa vipindi vyao.

labda napenda pia michezo ya fikra na kupingana kwa hoja kali na urafiki ukaendelea kuwepo

nafikiri nimekujibu @matondo

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"labda napenda pia michezo ya fikra na kupingana kwa hoja kali na urafiki ukaendelea kuwepo"

Nimependa sehemu hii ya jibu lako. Mimi ni shahidi. Wakora!

Kuhusu wachekeshaji, hapa wana "channel" yao nzima inayoitwa Comedy Central na ni moja kati ya Channel nizipendazo sana (pamoja na History na Discovery) kwani kucheka naamini ni muhimu. Wakianza vichekesho "vya kikubwa" basi hukimbilia katika kachumba fulani hivi na kufaudu huko peke yangu bila bugudha ya vibinti vyangu.