Friday, November 20, 2009

Them, I & Them.....NEW SONG......Nasio


"HALI YA UCHUMI WA DUNIA NI MBAYA"
Kauli hii tumeisikia mara kwa mara na imekuwa ikitumika zaidi ya UHALISIA wake. Ni kauli ambayo inatumika kuwatisha wananchi na pia kutumiwa na WATAWALA KUKWEPA MAJUKUMU YAO.
Hivi sasa kila kitu kisichokamilika chaonekana kuwa na sababu hii ya "mvurugiko wa uchumi". Hata wabunge hawatembelei majimbo ya (japo wanapaswa kuishi huko) sababu hii

  • Wananchi hawapati maendeleo sababu ya mvurugano wa uchumi.
  • Sera za serikali ya awamu ya nne hazikamiliki kwa sababu hiyohiyo
  • Sitashangaa nikisikia kiongozi akisema WANAKULA RUSHWA SABABU HIYO.
LAKINI KUNA UKWELI KATIKA KAULI HII?
Ukweli ni kwamba WANASIASA hawana mipango endelevu na sasa wanatumia hili la uchumi kuharibika kama kisingizio. Ni kweli kuwa kuna mambo yaliyokwamishwa na mvurugano wa uchumi, lakini bado kuna mengi tunayoweza kufanya kwa NGUVUKAZI na kuwezesha kuibadili jamii.
Kujenga zahanati, Kuchimba mitaro, Kuchimba visima, Kutokomeza Rushwa, Kuchonga / kutengeneza madawati na mengine kama haya ni baadhi ya mambo yanayohitaji nguvukazi na ushirikiano kati ya WATAWALA na wananchi.
HUU SI WAKATI WA KUTISHANA. NI WAKATI WA KUELEZANA MAJUKUMU YETU NA KUPANGA NAMNA YA KUYAKABILI. Na kwa kuyakabili kwa umoja (licha ya ugumu wake) tutafanikiwa na kujivunia. Hizi ni nyakati ambazo wanasiasa wanapaswa kuwaeleza wananchi kuwa HALI YA UCHUMI ISEMWAYO SI MWISHO WA DUNIA na kisha kuwaonesha mahala pa kwenda kutua mzigo wao wa msongo wa mawazo (stress)
Sijui ni kwanini kila wazungumziapo KUONDOA STRESS wanahusisha na mto, lakini ukweli ni kuwa KILA MTU ANA "MTO" WAKE ANAOWEZA KWENDA NA KUTUA MZIGO WAKE NA KUANZA UPYA MAISHA MAPYA, MAISHA CHANYA NA KUFANIKIWA.
Leo hii tunaye Nasio Fontaine anayezungumzia kuhusu kutambua ulipo "mto" wako kisha kuelekea huko "kutua mzigo wako" kisha kuanza maisha mapya. Anasema anajua MUNGU NDIYE SULUHISHO PEKEE HATA KAMA UNAHISI KILA KITU HAKIENDI VEMA KWAKO.
Msome na kumsikiliza katika wimbo huu NEW SONG


Yeah!, we really wanna say now.
Come down to the river, lay down your burdens,
walk away and singing a New Song, sing a Brand New Song
Come to Mount Zion Jah Seh, lay down your burden
Walk away and singing a New Song
Sing a brand new song

I know your burdens feels so heavy,
you feel you couldn't carry no more,
yet here comes another hurdle,
higher than the one before,
and i know the road you trod,
is rough and rugged,
still i know,
the Lion of the Judah is the only solution"

Come down to the river, lay down your burdens,
walk away and singing a New Song, sing a Brand New Song
Come to Mount Zion you heavy laiden, lay down your burden
cause you've been burden for much too long

Journey is tough, the road is steep
And there's no rest for weary feet.
Yet here come another stumbling block
Greater than the one before
And i know that you've been through
Soo Much, Too Much
And HARDER THE BATTLE, TOUGHER THE FIGHT
SWEETER THE VICTORY

Come down to the river, lay down your burdens,
walk away and singing a New Song, sing a Brand New Song
Come to Mount Zion Jah Seh, lay down your burden
cause you've been burden for much too long
For much too long

Come, come, come come, come to mount Zion
Lay down your burden
Cause in my Father's House
There is many a Mansion


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

4 comments:

Anonymous said...

Bado nasubiri ile HW ya honest scrap award...

chib said...

Tunashukuru kwa kutupa changamoto ya wikendi

malkiory said...

Hapa mheshimiwa umenigusa moja kwa moja. Siku zote nimekuwa nikilalamikia kitendo cha wanasiasa kutumia suala la mtikisiko wa kiuchumi kama kigezo cha kukwepa majukumu yanayowakabili ya keleta maendeleo. Mfano halisi ni waziri wetu wa fedha, oh, tumekumbwa na mtikisiko wa uchumi! Ama kweli hii ni dhana potofu.

徵信社 said...

I love it! Very creative!That's actually really cool.
謝謝你的文章分享,請你有空到我

參觀,Thanks!:))))