May 27 niliandika kuhusu suala la ku-Recycle baadhi ya vitu lilivyo muhimu na la lazima nchini Tanzania. Niliongelea namna kulivyo na mrundikano wa vuma chakavu kwenye sehemu mbalimbali (za serikali) kama vituo vikuu vya reli na vituo vikuu vya polisi mikoani (JIKUMBUSHE HAPA) . Na nikaeleza namna nchi nyingine zinavyonufaika kwa kufanya recycle ya vitu mbalimbali na zaidi vyuma. Wiki hii tumeshuhudia moja ya faida za ku-recycle baada ya kuwasili kwa meli ya kivita ya USS NEW YORK, meli iliyoundwa kwa kutumia tani 7.5 za vyuma vilivyobaki katika majengo ya World Trade Center kilicholipuliwa Sept 11, 2001 ambayo pia imegharimu dola Bilioni moja.
Ni kumbukumbu ya aina yake kwa wahanga wa tukio hilo. Wamepata nafasi ya kuiona meli ambayo ni KUMBUKUMBU HAI ya majengo na wale waliopoteza maisha yao na pia ni IMANI kuwa itaenda kupambana na kuwawajibisha wale waliohusika na tukio hilo.
Swali ni kuwa wasingekuwa na mpango huo wa ku-recycle, vyuma vyote vingeenda wapi???
Tunahitaji ku-Recycle mengi nchini mwetu

No comments:
Post a Comment