"Better to write for yourself and have no public, than to write for the public and have no self."
Cyril Connolly (1903 - 1974)
Monday, November 9, 2009
Za Kale vs Maisha ya Sasa....SIRI YAKO
Wengi tunajua kuwa kitu kikishaitwa SIRI basi ni cha kuweka mawazoni na kujitahidi kadri ya uwezo wako kutokisema kwa mwingine. Na kuna faida kubwa sana ya kutotoa siri (hasa kwa asiyehusika). Lakini vipi kuhusu UPANDE WA PILI??? Tumeshatafakari kuhusu FAIDA za mtu kuwa na mahala pa kutoa siri?? Tunaona wale wenzetu waendao KUTUBU kwa viongozi wao wa dini na kusamehewa "mizigo" yao na "kuwa huru" tena baada ya kutua siri hizo. Tunao wale wanaokwenda kwa wataalamu wa afya waliobobea kwenye mambi ya akili na ushauri kueleza siri na matatizo yanayowakumba na hivyo kutua mzigo mkubwa unaosonga akili zao. Lakini vipi kwa wale ambao wanaelezwa siri hizo na HAWARUHUSIWI kuzitoa?? Unadhani wanapokutana na matatizo kama hayo waliyoshauri ama kusikia watafanyaje?? Mfano mzuri ni Alhamis iliyopita ambapo mtaalamu wa ushauri katika jeshi la Marekani alifanya mauaji kwa askari wenzake 13. Kazi kubwa aliyokuwa akiifanya kwa miaka 4 ilikuwa kuwashauri askari warejeao toka vitani, ambao wametingwa na msongo wa mawazo (stress). Kwa askari hao kulikuwa na unafuu baada ya kuongea na "mtaalam" lakini kwa mtaalam alikuwa akizidi kurundika taswira mbalimbali za kutisha kuhusu vita (NILIYAJADILI HAPA). Sasa ilikuwa zamu ya Daktari huyu kwenda vitani kukutana na yote aliyosikia lakini hakuwa na mahala pa "kuyatua". Matokeo yake ni kuvuka mipaka ya ufikiri wa ki-utu na kufanya aliyofanya. UNADHANI ANGEKUWA NA MAHALA ANAPOPAAMINI NA KUTOA SIRI ZOTE ALIZONAZO ANGEFANYA ALIYOFANYA??? Turejee Jumatatuni na kukutana na wana Bima Lee katika wimbo wao, SIRI YAKO.
** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**
.Today we have bigger houses and smaller families; more convenience but less time. .We have more Degrees but less common sense; more knowledge but less judgment. .We have more experts but more problems; more medicine but less wellness. .We spend too recklessly, laugh too little, drive too fast, get too angry too quickly, stay up too late, read too little, watch Tv too much and Pray too seldom. .We multiply our Possessions but reduce our values; we talk too much, love too little and lie too often. .We’ve learned how to make living, but not a life; we’ve added years to life not life to years. .We have taller buildings, but shorter tempers; wider freeways but narrower viewpoint. .We spend more, but have less; we buy more, enjoy less. .We’ve been all the way to the moon and back, but have trouble crossing the street to meet our neighbor. .We’ve conquer outer space, but not inner space. .We split the atoms, but not our prejudice .We write more, learn less; plan more but accomplish less; we’ve learned to rush but not to wait; we have higher income but lower morals. .We build more computers to hold more info, to produce more copies but have less communications. .We’re long on quantity but short on Quality. .These are the time for Fast food and slow digestion; tall men and short characters. .More leisure but less fun; more kinds of food but less nutrition; two income but many divorces, fancier houses but broken homes.
3 comments:
labda hapana au sijui
Siri sijui kama kuna siri:-)
siri ni siri tu bwana
Post a Comment