Tuesday, November 10, 2009

Heri ya siku ya kuzaliwa Mamaaa

Mama wa Changamoto.
Wanasema kuwa mafanikio ya mwanaume mara nyingi huja kwa msaada mkubwa wa mwanamke wake. NAMI NAKUBALI.

Kama kuna kinachonifanya kusonga mbele nikiwa na tabasamu na tumaini basi ni mke wangu Mpeeenzi. Ambaye amekuwa msaada mkubwa niwapo na uchovu wa kiImani, kimwili, kiakili na kiuchumi. Na leo nakumbuka siku muhimu saana maishani mwake. Siku iliyoanzisha yote mema nijivuniayo maishani kutokana na uwepo wake. SIKU YAKE YA KUZALIWA.

Kama alivyoimba Beres Hammond,,,,,,kuwa naye kunaifanya dunia isiwe na makali iliyonayo na kunanifanya niendelee kujiona niko "peponi". Msome ukisikiliza kibao chake STILL WILL BE HEAVEN
If i'll live to see a hundred years or so,
And the ocean is now where green trees used to grow,
If suddenly everything just disappear
No where to go, no friends to see, house isn't there.
But if i look around and you are by my side
Every step i'll take, i'll take them all with pride
I'll sure miss this world and all it's rights and wrongs
I'll miss all the fun and all the beautiful songs
But
STILL WE'LL BE HEAVEN AS LONG AS YOU'RE THERE........
Happy Birthdate my Love a.k.a Mama P.

18 comments:

Anonymous said...

Heri kwa sikukuu ya kuzaliwa Mama Changamoto!

Fadhy Mtanga said...

Ni siku ya kuzaliwa,
Pongezi nyingi wapewa,
Heri nazo waombewa,
Mola atakujalia.

Ufanikiwe daima,
Kamwe usirudi nyuma,
Zidi kuwa mtu mwema,
Mube atafurahia.

Mola awape baraka,
Awaondolee shaka,
Pendo lisomithilika,
Ndiyo nguzo ya dunia.

Mary Damian said...

Happy Birthday mama Paulina!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijui kwa kihaya wanaimbaje ule wimbo wa happy birthday

waiyuka nokuzalwa iwe X3

waiyuka nokuzwalwa mama pau,

waiyuka nokuzwalwe iweeeeeeeeeee

swali; ainémyeka engahai?

Yasinta Ngonyani said...

Pongezi nyingi za siku hii ya kuzaliwa wifi mama P.Uwe na wakati mzuri kwa siku hii.

viva afrika said...

heri nyingi na fanaka zije kwako mama changamoto

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana mama wa changamoto, Mungu akuzidishie miaka.

** Da yasinta unamwambiaje Mzee wa changamoto kuhusu kumwita mkewe mama?

Yasinta Ngonyani said...

Da Mija nimeona Na nimeshangaa sana.Ila kusema kweli kwa mimi sitamwita mume wangu baba hata siku moja kwani yeye si baba yangu. Au labda Mzee wa Changamoto anataka uchokozi tu...LOL

Mzee wa Changamoto said...

Asanteni nyote.
Jamani Da Mija na Da Yasinta mbona kuna "a" tatu hapo?
Huyo si Mama bali ni Mamaaa. I wish ningeweza kuyaandika haya kwa note ili msome nisomavyo mimi muone tofauti.
Lol
Blessings to you all.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Happy Birthday mama Changamoto!

SHABANI O. KONDO said...

Kaka kwangu ni pongezi kubwa kwako kwa kumtukuza mkeo kwa namna hiyo kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku tusipowatukuza hawa wasaidi wetu katika masiha ni jambo baya na ninaimani hata mwenyezi mungu hapendi.

kiukweli fahamu msafiri hachoki endelea kuwa na shemeji yetu kwa amani na upendo.

Happy Birthday mama Changamoto.

Yasinta Ngonyani said...

Ok baba P. nadhani umeeleweka hapo heshima kwako.

Faith S Hilary said...

i think i am late!!! :-( but HAPPY BIRTHDAY MAMA P!!!!!!!!!

PASSION4FASHION.TZ said...

Happy birthday mamaa!!! na hongera sana kwa kazi nzuri unayoifanya,matunda yake tunayaona na wengi tunayafaidi...lol.

John Mwaipopo said...

hongera kwa siku ya kuzaliwa mama yetu. kokwa la tunda ulilokula kusherehekea miaka hiyo uliyonayo litoe mti na huo mti ufike miaka mia moja ndipo ule tunda lake tena.

chib said...

Mimi nafikiri sijachelewa nikisema heri katika siku yako ya kuzaliwa Mama P!

Simon Kitururu said...

Heri ya kuzaliwa mama P!

Na usichoke kutufinyia huyu kaka yetu ukihisi uzembe!:-)

dina marios said...

mwenyezi mungu awabariki nakuwazidishia heri na baraka tele hasa katika kipindi ambacho familia imekuwa,najua nimechelewa kuacha ujumbe wangu hapa..heri ya siku yako ya kuzaliwa wifi yangu Mama Paulina..ubarikiwe sana.