Thursday, December 3, 2009

2010 kuwa na rekodi ya "wazee" kwenye Heavyweights

Bernard Hopkins enzi zake akiwa na mikanda yake
Evander enzi za enzi. Je wataweza kurejesha makali haya?
Mwaka 2010 unaweza na rekodi ya kuwa na "wazee" kama mabingwa wa Dunia endapo nyota waliotawala mchezo huo kwa miongo kadhaa Bernard "The Executioner" Hopkins na Evander "The Real Deal" Holyfield watashinda mapambano yao mawili wanayokabiliana nayo mbeleni.
Hopkins ambaye usiku wa kuamkia leo alishinda pambano lake la raundi 12 dhidi ya Enrique Ornelas, ameonesha nia ya kuwania taji alilonalo David Haye ilhali Evander atakayepambana Jan 16 huko Uganda dhidi ya Francois Botha huku akiwa anawaza kupanda ulingoni mwishoni mwa mwaka 2010 kuwania mkanda wa WBC alionao Vitali Klitschko.
Hopkins atakuwa na miaka 45 mwanzoni mwa mwakani ilhali Evander ana miaka 47 sasa hivi.
Bondia George Foreman ndiye anayeshikiliza rekodi ya bondia mwenye umri mkubwa zaidi alipochukua mkanda akiwa na miaka 45 alipomshinda Michael Moorer kwa KO mwaka 1994.
Evander aliyeanzia kwenye uzito wa Cruiserweight, anashikilia rekodi ya kuwa bingwa wa Dunia uzito wa juu mara nne na anasaka rekodi ya tano.
Hopkins yeye alikuwa bingwa asiyepingika katika uzito Middleweight kwa zaidi ya miaka 10 kabla hajaamua kuongeza uzito kwenda Light Heavyweight na sasa anasaka mkanda wa Heavyweight.
Yetu macho na kila la kheri kwao wote

No comments: