Wednesday, December 16, 2009

Hatimaye DREAMLINER yagusa anga

Picha toka http://www.aviationspectator.com Chumba cha marubani.....Cha kisasa zaidi. Picha toka http://www.flightglobal.com Wafanyakazi wa Boeing wakishangilia
Ikifuatiliwa na "chase plane" Picha zote tatu toka http://www.dailymail.co.uk
Binafsi si mpenzi wa kusafiri kwa ndege. Sina hisia nzuri ninayokuwa nayo ninapokuwa kule. Yaani kuwa angani nafikiria "kama ndege ikipata stroke" na mambo kama hayo. Lakini tukitua huwa nafurahi kufika mapema na salama kuliko ambavyo ingekuwa kwa gari ama baiskeli. Lakini katika vitu napenda kufuatilia ni mambo ya anga. Kuanzia NASA, miundo na utendaji kazi wa ndege, mabadiliko yake na hata gharama ikiwezekana. Pia kazi hii ya ndege ndio inilishiayo minyoo yangu na familia yangu. Kwa maana nyingine, ndio iletayo mkate wa kila siku. Baada ya kucheleweshwa kwa zaidi ya miaka miwili na nusu, hatimaye ndege hii imefanya jaribio lake la kwanza. Leo nilikuwa nimekaa mbele ya Tv nikiangalia kuruka kwa ndege hii ya Boeing 787 iliyopewa jina la DREAMLINER. Ni ndege mpya na ya kisasa toka BOEING ambayo imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa kwa kutumia malighafi za CARBON na TITANIUM yanayoaminika kuifanya kuwa nyepesi na itakayosaidia kupunguza gharama za mafuta. Leo imeanza msururu wa majaribio ambao huchukua takribani robo tatu mwaka kukamilika ukirusha na kukusanya takwimu za urukaji wake. Yategemewa ndege ya kwanza kimauzo itaenda Japan.
Binafsi nafurahia kuona inakwenda angani kwani nasi tumeshiriki kutengeneza vipuri vya ndege hizi (nasema hizi kwani hatujui zaenda ndege ipi na najua wana zaidi ya moja tayari kwa kuruka)

8 comments:

Anonymous said...

te teh teh, ikipata 'stroke' na wewe una-stroke nayo tu na hivi imetengenezwa kwa elementi zenye uzito mdogo, mbona ikistroke ndo itaserereka kwa kasi ya karatasi sasa? LOL ha ha hah Mube, acha woga. Saasa bwana, mi nashukuru kwa kutufahamisha. Thx!

Mzee wa Changamoto said...

Subi... Hivi kuna dawa ya woga?
Maana hata nifanyeje, huwa najiuliza "hivi hili dubwana halichokagi tu?" Ukisema ni jipya nasema "halina uzoefu" ukisema lina usoefu nasema "lishachoka"
Yaani ni uoga kwa kwenda mbele
Lakini haya yote yanakuwa ndani kwa ndani. HUWEZI KUYAONA USONI. Huwa nina-fake smile mpaka unaweza kunipa tuzo ya abiria anaye-enjoy safari kuliko yeyote yule.
Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa
Ila napenda saana kuwaangalia. Hasa zile SPACE SHUTTLE zinapoondoka na kutua na wanapokorokochoa huko juu, napenda kwelikweli kuwaangalia na kuwa-interview lakini kwenye suala la kuingia humo na mie niende nao?????? AAAAAAAAAAHHHH WAPIIIIIIII

Godwin Habib Meghji said...

Hii ni hatua nzuri sana kwa kampuni ya Boeing. niliwahi ku-google muda fulani( ni kama miaka 2 iliyopita) ku compare Boeing na Airbus. Vitu nilivyosoma nilijikuta ninapokata ticket ni lazima nijue ni aina gani ya ndege nitapanda. Nipo tayri kuahirisha au kubadilisha kampuni ya usafiri ili mradi ndege iwe ni airbus. Na ninapokuwa kwenye airbus ninajiona salama zaidi, Ingawaje kale kauoga kapo kapo ila huwezi kufananisha kama nikipanda Boeing. Na ukweli hata katika soko Airbus wanafanya vizuri kuliko Boeing haswa kutokana na gas consumption. Kutokana na data za wataalamu wengi airbus ni salama zaidi kuliko aina nyingine za ndege. SIJUI LOLOTE KWA HILI

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kijana mmoja alipaswa kusomea ufundi wa magari, meli au ndege. babaye akamwambia asomee wa magari kwani gari lipo ardhini siku zote. sasa ndege ukikarabati isikarabatike huku angani mtaenda wapi? au meli itasimama wapi? lakini gari liko ardhini waweza ruka chin nk.

acha uaoga, usiogope kifo kwani huendi kufa bali unasafiri kwenda uedako. fikiria kufika na usifikirie kifo, huendi kifoni japo kifo ni haki yako ya msingi

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Kamala. NDIO MAANA NIMEULIZA HIVI KUNA DAWA YA WOGA??? Natamani kupenda kusafiri japo sijui namna nitakavyoweza kupenda.

Kaka Godwin, kama ulivyosema hii ni hatua nzuri saana kwa Boeing ambayo sasa imeonekana kuipiku Airbus kwa hii ndege (http://www.smarttravelasia.com/AirbusVsBoeing.htm). Lakini tunastahii kuwa makini tunapo-compare hivi vitu hasa kwa huku ambako kuna baadhi a critics wanakuwa na "locked mind" katika baadhi ya vitu. Ama wanakuwa wanafanya GENERAL COMPARISON ya makampuni bila kujali ni ipi ina ndege nyingi ama ipi ina mali nyingi. Binafsi kabla sijaanza kushughulika na utengenezaji wa vipuri vyao sikuwa najua makampuni mengi ya ndege. Lakini sasa najua kuwa kwa size ndogondogo sidhani kama Airbus wala Boeing wana nafasi ya kuzipita Cessna na Gulfstream. Hizi zinafanya vema saana huko kwenye videge vidogo. Ukienda kwenye ndege za kivita utakuta Lockheed Martin wanayoyoma na kushindana na kampuni ningine (imenitoka kichwanbi) na sasa huku kwenye midege ya abiria mikubwakubwa ndio unakutana na hawa wawili wapendanao.
Ndivyo ilivyo kwenye chakula hapa ambapo japo si kila mlo wa Mc Donalds unashauriwa, lakini kwa ujumla wanafanya vema. Japo zipo fast foods zenye milo iliyo ya ki-afya zaidi na inayoshauriwa na wataalamu. Ama kwenye computer ambapo licha ya jina kubwa na mauzo mwanana, DELL si kampuni ambayo wataalamu wengi wa IT wanamiliki laptop zake. Wanajua kuwa jina ni kubwa kuliko ubora. Ama kwa sisi "walevi wa picha" tunajua kuwa licha ya kuwa na jina kuuubwa, SONY hawana lolote kwenye kamera kuwa za SLR. Lakini ukiweka ujumla wake, wanafanya vema (kwa jina) na wanaweza kuonekana wako juu.
Pengine sasa katika kulinganisha hawa watu, inabidi uende kwa size zinazoshabihiana. Mfano Airbus380 vs Boeing 787. Ama Airbus A330 vs Boeing 767 au Airbus A340 vs Boeing 777 nk.
Kwani kuna ambazo Airbus wako juu na ambazo Boeing wako juu na ndio maana wote bado wako kwenye biashara kutokana na ubora katika sehemu fulani
Blessings

Markus Mpangala. said...

SINIA LA ELIMU HILO KAKA, KWA HAKIKA WOGA NI GONJWA BAYA MNO

Godwin Habib Meghji said...

Nimekusoma, shukrani kwa darasa. itabidi niongeze shule hii kwa kuingia maktaba

Anonymous said...

Haijagundulika bado dawa ya woga. Wanachofanya ni kukupa dawa ya kukulaza tu ili muda upite usijue kinachotokea. Ingekuwepo dawa ya kuzuia woga, basi watu maarufu wenye ugonjwa wa kuogopa (phobia) wangeshazitumia, unamkumbuka Dennis Bergkamp? alikuwa hasafiri wakati timu yake ya Arsenal ikicheza mechi zinazohitaji kupanda ndege, ndiyo maana mechi zake za kimataifa chache na hizo aliweza kuzicheza pale alipokuwa na muda wa kusafiri kwa gari au merikebu kabla ya siku ya mechi.