Thursday, December 31, 2009

Heri ya mwaka mpya na wenye mafanikio 2010


"SUCCESS is not measured only in ACIEVEMENTS.......but in LESSONS LEARNED, LIVES TOUCHED AND MOMENTS SHARED ALONG THE WAY"
Hii kwangu yaweza kuwa fafanuzi nzuri zaidi ya MAFANIKIO ninayoifahamu. Ni kweli kuwa mafanikio hayapimwi kwa kile kionekanacho pekee. Bali hata mafunzo tuliyopata katika kupambana na harakati za maisha yetu kila siku. Na kama mafanikio yanahusisha mapambano na mafunzo na ushirikishi tunaokuwa nao katika maisha yetu, binafsi nasema NIMEFANIKIWA.

Nasema nimefanikiwa kwa kuwa NIMEJIFUNZA MENGI kuhusu maisha kwa kujuana na kuelewana na wengi katika ulimwengu hasa huu wa ku-blog na pia nimeweza kushauriana mengi kuhusu mambo mbalimbali ya maisha hivyo nasema nimegusa maisha na mwisho nimeshirikishwa katika matukio mbalimbali jambo linalonifanya niamini kuwa nime-share moments katika kila nililoshirikishwa.

Lakini kubwa ni kuwa NIMEFANIKIWA kwa kuwa nimeweza na naendelea kukabiliana na haya magumu ya maisha. Wapo wanaoshindwa kuwa na shukrani kwa Mungu kwa kuwa wanaamini mwaka unaoisha umekuwa mgumu na pengine ujao hautakuwa na tofauti. Sina ninaloweza kufanya zaidi ya KUMSHUKURU MUNGU kwa mwaka huo huo mgumu kwani nimeufikiwa kwa mapenzi yake, nimo ndani ya mwaka huo mgumu kwa mipango yake, napigana na magumu hayo kwa msaada wake na nitayashinda kwa kudra zake.

Pengine lolote nililojifunza katika kukabiliana na mwaka huu ni MAFANIKIO kama ambavyo alizema Orison Swett Marden alipotafsiri mafanikio akisema “Success is not measured by what you accomplish, but by the opposition you have encountered, and the courage with which you have maintained the struggle against overwhelming odds.”

Na sasa ni wakati wa kuanza kuangalia upya maisha yetu. Kuangalia upya mafanikio na kumshukuru Mungu kwa uwezo anaotupa kuweza kukabiliana na yale yatukumbayo. Ni kwa kufanya hivi tutaweza kuridhishwa na kile kidogo tufanyacho na kisha kupata nia ya kufanya vema zaidi. Tunastahili kufuta dhana kwamba mafanikio hupimwa kwa pesa pekee kwani furaha halisi si kwa pesa, bali kuwa na uwezo wa kufanya kile tupendacho kama ambavyo Bob Dylan alisema kuwa "What's money? A man is a success if he gets up in the morning and goes to bed at night and in between does what he wants to do."
Tujipange vema, tujithamini na kisha tutende yaliyo mema na yaliyo na nia halisi mioyoni mwetu na hapo tutazidi kufanikisha.

TUSHIRIKIANE, TUPENDANE, TUJALIANE NA TUTHAMINIANE.

Blessings
Nimekumbuka saana nyumbani. Nyakati kama hizi ni safari safari tuuu na ni kumbukumbu hiyo iliyonifanya nikumbuke mkusanyiko wa clips zangu za safari ya Zanzibar kwa kina Da Naniliiiuuu. Waweza kuiangalia ila kumbuka kuwa ni VIDEO YA SAFARI. Kwa hiyo unasafiri nami zaidi ya kujua kilichonipeleka
Lol
Love y'all.

3 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Hongera wee kwa kwenda Zenji

Ujumbe mzito huuu!

Yasinta Ngonyani said...

Heri ya mwaka mpya na pia uwe na mafanikio kwako pia. Mwaka 2010

chib said...

Mzee, heri ya mwaka mpya 2010