Na Judith Mhamaka
Morogoro
MAAFISA ushirika katika wilaya na mikoa yote wameshauriwa kuwaelimisha wakulima ili kuweza kujiunga katika vikundi na kuunda vyama vya akiba na mikopo ili kuwezesha kufanikisha mkakati wa kilimo kwanza nchini.
Ushauri huo umetolewa jana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kuendeleza kilimo kwa kutumia zana (DEMACO) Kaya Kazema wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi .
Alisema kuwa kilimo kwanza hakitoweza kuwa endelevu iwapo maafisa ushirika hawatakuwa karibu na wakulima kwa kuwaunganisha pamoja na vikundi ili kuweza kuwafanya kupata mikopo.
Alisema kuwa ili kuweza kupata mikopo mbalimbali ikiwemo ya kilimo, wakulima wanatakiwa kujiunga katika vikundi vitakavyowawezesha kuunda SACCOS zao na pengine kuunda mpango wa stakabadhi mazao ghalani ambao pia utawawezesha kupata mikopo kutoka mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.
Alisema DEMACO wanaukubali vizuri mfumo wa stakabadhi mazao ghalani kwani unauwezo mkubwa wa kumfanya mkulima kulipa kwa wakati mkopo aliokopa kufuatia mazao atakayolima kuhifadhiwa kwenye ghala la husika hivyo stakabadhi ya mazao ghalani iendelezwe.
Aidha alisema, moja ya masharti yao ya mikopo kwa kushirikiana na taasisi za fedha wakulima wanazungumzia zaidi wenyewe malipo yao kwa awamu ngapi kutokana na aina ya kilimo anachokifanya hivyo kuwa nauhakika katika ulipaji wa mkopo kulingana na makubalino aliyoingia.
Kazema alisema kuwa hiyo humfanya mkulima mwenyewe kuwa makini katika kurejesha marejesho ya mkopo na kuondokana na dhana ya kurejesha dhamana ya mkopo ambayo ni mali aliyokopa pindi akishindwa kurejesha ambapo alisema stakabadhi mazao ghalani itakuwa ni rahisi kumfuatilia mkulima na kurejesha kwa wakati.
Alisema kuwa ikiwa maafisa ushirika hao watafuatilia kuunda vikundi hivyo na hatimaye SACCOS watasaidia mikoa ya G8 ambayo inazalisha chakula kwa wingi na hivyo kufanikisha mpango wa kilimo kwanza.
Aliitaja mikoa ambayo inazalisha chakula kwa wingi kuwa ni Ruvuma, Morogoro, Singida, Rukwa, Kigoma, Dodoma , Mbeya na Iringa na kufanya dhana ya kilimo kwanza kuwa endelevu.
Kampuni ya DEMACO inatoa mikopo ya matrekta makubwa na madogo kwa kuwasaidia wakulima kupitia SACCOS zao kupata mikopo ya zana za kilimo kupitia benki mbalimbali zinazokubalika na DEMACO ambapo tayari imeshatoa matrekta 15 yakiwemo makubwa na madogo katika mkoa wa Morogo
HABARI KWA MUJIBU WA MDAU Merina Robert
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment