Sunday, December 20, 2009

Wamasai waeleza kuhusu kazi ya ulinzi na biashara ya dawa

Na Judith Mhamaka
Morogoro

KUMEZUKA wimbi kubwa la vijana wa jamii ya wafugaji hasa wa kimasai kujihusisha na biashara ya uuzaji wa dawa za miti shamba na ulinzi hali ambayo imezua mtizamo tofauti kwa jamii huku wengine wakidai kuwa huenda tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji imechangia hali hiyo.

Kisongo Nguso Timbila ni mfanyabiashara wa dawa za asili kutoka jamii ya wafugaji wa kimasai katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa wameamua kujiingiza katika biashara ya dawa za asili kufuatilia kuzuka kwa magonjwa mengi ikiwemo kisukari,shinikizo la damu,figo ,kuuma miguu na mengine hivyo wakaona kuna haja kwao kuisaidia jamii kutatua matatizo hayo kutokana na kuwa na utaalamu huo katika kutibu magonjwa hayo kwa kutumia dawa za asili.

Timbila alisema katika biashara hiyo imekuwa wakiifanya vizuri na imekuwa ikiwaingizia kipato kizuri na kumwezesha kuendesha maisha yake na kiasi kingine kupeleka fedha hizo kwa baba yake huko wilayani Nkinga mkoani Tanga na kununulia mifugo yake.

"si kwamba sisi kuja mijini kufanya biashara ya kuuza dawa za asili inamaanisha kwamba huko tunakotoka hakuna mifugo si kweli bali ni kutoa tiba hiyo kwa wenzetu ambao wamekuwa wakisubuliwa na magonjwa hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na kuwaathiri walio wengi''alisema Timbila.

Mfanyabiashara huyo wa dawa za asili akizungumzia suala la kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara hiyo ambao si wakweli katika tiba hiyo alisema kweli kumekuwa na watu wa aina hiyo lakini si wote kwani iwapo utakuwa muongo lazima utabainika kwa wateja unaowauzia dawa hizo kutokana na matokeo atakayoyapata mteja.

"kweli wapo watu wanasema wana dawa za kuongeza nguvu katika kufanya mapenzi lakini hiyo si kweli hali hiyo inawatokea baadhi ya watu kutokana na kukabiliwa na magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu lakini si kweli kuna dawa hizo ila kwa kutibu sukari au shinikizo la damu kunasaidia kumuondolea hali hiyo anayesumbuliwa na matatizo hayo"alisema Timbila.

Akielezea juu ya suala la baadhi ya vijana kufanya kazi ya ulinzi alisema baadhi yao inatokana na uvivu kwa baadhi yao katika kuchunga mifugo kijijini kwao lakini wengine wamekuwa wakitafuta fedha kwa ajili ya kununulia mifugo na pale yanapofikia malengo yao basi hurejea kijijini na kuendelea n ufugaji.

"unajua sisi wafugaji huwezi kurithi mifugo kabla baba hajafariki hivyo sasa katika kujipatia mifugo yetu wenyewe ndio unakuta wengine tunajiingiza katika shughuli za ulinzi ili kuweza kupata fedha za kununulia mifugo ya kwetu wenyewe kwani baada ya kupata fedha huzituma kijijini kwa ajili ya kununulia mifugo hiyo"alisema Timbila.

Kijana huyo alisema si kwamba zoezi la uhamishaji wafugaji katika maeneo ya Kilosa na mengineyo ndio yamechangia wafugaji vijana kuja mijini na kufanya biashara ya dawa za asili au ulinzi huo ni mtazamo wa baadhi ya watu lakini si kwa vijana wa kifugaji.

HABARI KWA MUJIBU WA Merina Robert

No comments: