Monday, December 14, 2009

Za Kale vs Maisha ya sasa........Mv MAPENZI II

Novemba 11 mwaka jana niliandika kuhusu wimbo huu. Lakini ulikuwa kama mfano kwa wasanii wa Bongo Flava ambao wanaonesha kutokuwa wabunifu katika kueleza hisia na lawama zao kwa wawaelezao na matokeo yake kufanya nyimbo kuwa "majibizano ya ana kwa ana" kuliko uburudishaji na uelimishaji. Niliamua kuweka unafiki kando na kuwaleza wazi kuwa Iwe "bifu" la kweli ama "gemu". Ubunifu bado ni ziro (Isome hapa)
Nilieleza mengi kuhusiana na nyimbo zetu zilizonanga waliohusika na kupeleka ujumbe tofauti na wa kuelimisha kwa wasiohusika. Na hapa ndipo tunapoheshimu kazi za Fanani kwa hadhira. Kupeleka ujumbe sawa kwa mhusika hataka kama ni wimbo mmoja, wahusika tofauti na jumbe tofauti. Ntanukuu sehemu niliyowaeleza Bongo-Flavans nikisema "zamani nyimbo zilikuwa zina picha ambayo kama ulikuwa ukijua kinachoendelea basi ungejua kinachozungumzwa na kama hujui kinachojibiwa hapo unakuwa na taswira nyingiiine kabisa tena yenye mafunzo tofauti na mema kwa jamii. Kwa wale ambao hamkuwahi "kuchimba" maudhui halisi ya nyimbo, mnakumbuka MV. Mapenzi II ya Sikinde? Mnajua ilikuwa dongo kwa walioikimbia Sikinde kwenda kuanzisha Safari Sound? Je Chatu Mkali iliyowajibu Sikinde? Unakumbuka nyimbo Msafiri Kakiri ya Juwata? Unajua ilikuwa ni ujumbe kwa nani? Na Talaka Rejea ya Sikinde? Unajua lilikuwa jibu kwa nani? Lakini kama hujui kuwa kuna majibizano katika nyimbo hizo, huoni pia kuwa kuna mafunzo ya tofauti kwenye Mv Mapenzi inayoelezwa kama meli kwenye bahari yenye dhoruba, ama Chatu na sifa zake za uwindaji msituni, ama mtalakiwa anavyoeleza juu ya talaka rejea aliyopewa? Kwa taarifa yenu, hayo yote yalikuwa madongo lakini bado yalifikisha ujumbe kwa wahusika, yakaelimisha wasiohusika na ndio maana nasema watunzi wetu wa zamani walikuwa makini katika kazi zao na licha ya kuwa na zana duni za kutendea kazi, bado waliweza kuwa na ubunifu wa hali ya juu."
Sasa kwa kuwa tumesharejea MAUDHUI ya wimbo huu wa MV MAPENZI II, na tuusikilize na kuburudika tukijivunia ubunifu mkubwa wa wanaSIKINDE. DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA. Sikiliza UJUMBE kamili kwenye "Radio Call" yao. Ni Ujumbe, Muziki mtulivu na kisha wanarejea kwenye shangilio baada ya "over and out"...Hahahahaaaaaaa. Zamaniiii ilikuwa raha.

NB: Bado "nababatiza" muziki baada ya host wangu kutukimbia bila taarifa. Kama player haijacheza wimbo, waweza kuusikiliza moja kwa moja HAPA
** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia siku za Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**

1 comment:

Bennet said...

Ugomvi wa zamani ulikuwa burudani kwa sababu walipigana vijembe kwenye nyimbo tu basi, lakini sasa hivi utasikia wamepigana ngumi ukumbini, fujo tupu