Sunday, January 10, 2010

Dunia ina mambo...... We acha tuuuuu!!!!!!

Ni wikiendi na tunaigeukia dunia na mambo yake
DUNIA INA MAMBO!!!!!
Kila kukicha tunakutana na taarifa na habari ambazo zinatufanya tuwawaze watendaji kuwa WALIWAZA NINI? Na ndicho kipengele kitujiacho siku za mwisho wa wiki kutupumzisha tukiburudika na kuelimika kuhusu wenzetu ambao wanafanya mambo ambayo wengine wanayashangaa.
Lakini si yote ya kushangaza kwani hili lifuatalo lasikitisha zaidi. Mama mmoja mkazi wa hapa Washington DC Metro alifanya la ajabu alipojaribu kumuiba mtoto aliye tumboni. Alichofanya ni kumlaghai mama mjamzito asiye na makazi maalum (homeless) wa huko DC kuwa atampatia nguo za watoto na kumpeleka kwake ambako alimfungia kwa siku tano. Baadae alitumia kiwenbe na kisu cha kukaria maboksi kumkata Mama mjamzito ili aweze kumtoa mtoto na kumchukua. Hakuweza kufanikiwa kufanya "UPASUAJI" wake na kuamua kwenda kujipumzisha. Ndipo mwanamama huyo alipofanikiwa kutoroka huku utumbo na mfuko wa uzazi vikiwa vinaonekana. Alisaidiwa na kupelekwa hospitali. Hatimaye mtoto alizaliwa salama na kupewa jina la MIRACLE. Mama na mtoto wanataraji kupona na kuishi. Waweza kusoma habari kamili kwa kuBOFYA HAPA ama angalia video ya maelezo ya ukatili wake hapa chini

View more news videos at: http://www.nbcwashington.com/video.


Na katika kile kilichoonekana kama maendeleo, sasa hivi "wataalamu" wamegundua na ku-design electronic guitar ambayo imeundwa ndani ya t-shirt. Ina maana hakuna kubeba ma-amplifier wala nini. Ni kila kitu mumo kwa mumo. Sijui kiafya inakuwaje na wanaocheza na kubuni WALIWAZA NINI?
Angalia vijana wakifanya "concert" isiyo rasmi kwa kutumia magitaa hayo. Ila nao sijui waliwaza nini kufanya tamasha lao chooni? Lol
Tena mwenzao aliyemaliza haja ndogo hata hakuosha mikono. Sijui aliwaza nini? Duhhhhh!!!!!

Na mwisho ni haya mashindano ambayo washiriki huigiza kupiga gitaa lisilokuwepo. Wenyewe wanaita AIR GUITAR na ni mashindani yanayofanyika kila mwaka. Yana mashabiki ulimwengu mzima na kati ya washiriki wapo walioifanya hii kuwa full-time job ambayo inawaendeshea maisha yao. Video ya mshindi wa mwaka jana si nzuri kwa kweli nimeona nikuwekee hii ya mwaka 2008. Lakini waza wanapojifua na kuingia mashindanoni WANAWAZA NINI?


***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya "UJINGA" na kujikuta wakiingia matatani ama ambao wanafanya yanayoishangaza jamii. Wale watendao ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

4 comments:

Born 2 Suffer said...

Huyu ni mpumbavu na anaroho ngumu kumpasua mtu na kumwacha hivyo kweli duniani kuna mambo.

EDNA said...

Dunia imekwisha,tumeona na kusikia mengi lakini hilo la kumchana mtu tumbo balaa,wamchunguze akili huenda akawa na matatizo ya akili.

Faith S Hilary said...

Mmh mh mh mh mh mh...huyo mama mjamzito ndio mh mh mh mh...yaani nimeshangaa mpaka duh...ok no further comment

chib said...

Habari ya mama mjamzito inasikitisha sana