Saturday, January 9, 2010

Happy Birthdate Sis

Wakubwa zangu Dada Ninsy (kulia) na Dada Ajuna wakiwa na Mama yetu mpenzi(kati)
Nikiangaza maisha yangu, najivunia wakubwa wangu wawili hapo juu walioambatana na Mama. Ndio Dada zangu walionitangulia. Na leo, Dada Mkubwa-Mdogo Ajuna ndiye akumbkaye siku ya kuzaliwa. Huyu ndiye "aliyeniachia titi" na pengine ndiye niliyeishi naye kwa muda mrefu zaidi ya ndugu wengine. Ndiye niliyekwaruzana na kuelewana naye zaidi na ndiye aliyeonekana kuwa karibu zaidi pia.
Dadangu huyu alikuwa mfano-hai wa maisha kwa namna alivyopambana na pilika za maisha baada ya shule na alifungua njia ya kujaribu kwangu.
Katika siku yako muhimu leo, NAPENDA KUKUTAKIA KILA LA KHERI, BARAKA TELE NA MAKUZI MEMA YA "WAJOMBA"
Wajua TWAKUPENDA NA TWAKUOMBEA na TUNAJIVUNIA UNAVYOENDELEA KUWA MFANO KWA WENGI
Baraka kwako na kwa familia nzima.

HAPPY BRITHDATE DADA AJUNA

7 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Hongera Ajuna! Ubarikiwe sana!

Mija Shija Sayi said...

Hongera dada Ajuna, uwe na siku njema.

Mmefanana na Ajuna.

Stay blessed.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana dada Ajuna, nakutakia maisha marefu na mafanikio mema katika maisha yako. Ni kweli mmefanana huwezi kubisha kuwa sio ndugu. Ubarikiwe sana

Mwanasosholojia said...

Hongera dada ajuna, hongera Mzee wa Changamoto kwa kuwa na dada wa mfano!

EDNA said...

Mungu na akuongezee miaka mingiiiiiiii, HAPPY BIRTHDATE Dada.

Faith S Hilary said...

Yaani nobody will ever "argue" that it is your sister! Yaani mlivyofanana wote...do you have a picture mliopiga wote pamoja? Should be a great one...anyway Happy Birthday dada Ajuna. I hope your brother sends you these wishes we all write here...(mmh)

mumyhery said...

Happy birthday dada