Friday, January 15, 2010

Happy Birthdate Brother Simon Kitururu

Picha toka ukurasa wa Kaka Simon wa "usokitabu" aka facebook (Bila ruhusa. Kwi kwi kwiiiiiii)
Labda
kila siku ni ndefu kuliko unavyoweza kuidhania.
Ama
hatuthamini siku kwa kuwa tunadhani ni HAKI yetu kuiona kila dakika iliyo mbele yetu
Ila
twasahau kuwa katika kila sekunde kuna maelfu washindwao kuiona siku nyingine.
Nirejeshe Porojo.
Leo nimesikia habari ya Baba mmoja toka New York ambaye alifika Haiti saa 3 na robo asubuhi ya Jumanne, akaingia hotelini na kupanga mipango ya kesho na kisha kula, akaenda kulala na tetemeko lilimkuta hapo. Mamia wamepoteza maisha ndani ya hoteli ila yeye alipona japo hataweza kutumia tena miguu yake
Nililojifunza
ni kuwa ndani ya siku moja maisha yanaweza kubadilika kwa wengi. Yanaweza kuwapoteza na kuwaongeza wengine. Na kuwa siku moja yaweza kutoonekana kuwa ndefu kama ni ya kawaida kwako. Walio Haiti wanaweza kujua jinsi siku ya Jumanne ilivyokuwa ndefu.
Ndio maana NAMSHUKURU MUNGU KWA MWAKA ULIOUKAMILISHA LEO NA NAOMBA TUZIDI KUZITHAMINI SIKU ZA MAISHA YETU
HERI YA TAREHE YA KUZALIWA KAKA
Sina hakika na miaka ila najua ni mmoja zaidi ya jana. Pengine ukiangalia nyuma unaona makosa uliyofanya, unaona ambalo unatamani ungefanya tofauti, unaona ambalo hutaki kurejea kulifanya. Na hapo ndipo linakuja suala la ku-make wish. Hebu nirejee asilini (si umeona kwa Koero? Lol) kukusikilizisha country ya Darius Rucker akizungumza alivyo-make wish yake akisema kuanzia sasa "am gona work like i don't need no money, am gonna laugh like i'm not afraid to cry, i'm gonna dance like nobody is watching. Am gonna love while i still got the time." Sikiliza maneno zaidi hasa siku yako hii ya kukumbuka tarehe uliyoambiwa umezaliwa.
So, What's your wish?

Katika lolote upangalo, na ufanikiwe ili tuendeleze burudani, uelimishaji na ukombozi kwa jamii. Just KEEP ON MOVING

HAPPY BIRTHDATE BROTHER

11 comments:

mumyhery said...

Happy Birthday Simon, Mungu akuzidishie umri mrefu, afya njema na akujalie baraka zake kwa kadri ya mahitaji yako

Anonymous said...

Happy Birthday SIMON
Mungu akutangulie katika kila jambo


disminder

Anonymous said...

Happy Birthday SIMON
Mungu akutangulie katika kila jambo


disminder

Born 2 SUffer said...

Happy Birthday mwanawani (SIMON) umefikisha miaka mingapi? anyway mola akuzidishie umri mrefu maishani mwako.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa siku ya kuzaliwa. Mungu akulinde.

Fadhy Mtanga said...

naomba nami nikutakie heri ya siku ya kuzaliwa. uwe na furaha, amani na mafanikio.

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana Simon.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Hongela!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

katururuuuuuuuuuuuuu

Simon Kitururu said...

Asanteni wote hasa Mzee wa CHANGAMOTO kwa kunikumbuka!

Asanteni sana tena sana!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mwanafalsafa Mtakatifu naye anasherehekea birthday? Kweli?

Happy birthday mkuu....