Sunday, January 17, 2010

Meli tatu za kuokoa maisha Haiti

Mwisho wa wiki hii hatutakuwa na kipengele chetu cha WALIWAZA NINI, bali naendelea kuwawaza ndugu wa Haiti. Na sasa nilipokuwa napitia shughuli za uokozi, nikakutana na hii ya meli hizi tatu kubwa ambazo zitashughulikia uokozi na ukarabati huko Haiti.
Meli ya kwanza ya kijeshi ya USS CARL VINSON

Image from Web Shots.com
Imeshawasili nchini Haiti na itatumika kama kiwanja cha ndege kwa helikopta 19 ilizobeba ambazo zitatumika kusambaza msaada. Pia itakuwa na zaidi ya wanajeshi 3000 na ina uwezo wa kusafisha maji maelfu ya lita kwa siku ambayo yatapelekwa kwa wahitaji. Kwa mujibu wa mtandao wa The Wall Street Journal uliofanya mahojiano na nahodha wa meli hiyo Capt Bruce Lindsey, yanasema The Vinson brought an expanded complement of 19 helicopters to Haiti, and Capt. Lindsey said the ship will function as a “floating airport” for helicopters picking up supplies from other ships or from a new logistics hub at Port-au-Prince’s international airport and then flying the supplies into hard-to-reach areas of Haiti.
One of the largest ships in the American fleet, the Vinson also carries equipment capable of purifying large quantities of water and has extensive medical facilities, including two surgical rooms and dozens of hospital beds. It will be used to treat wounded Haitians until the Bataan and the Comfort arrive next week.

Meli nyingine ni USNS COMFORT
Image from Kobus' Picasa Gallery
Ni hospitali eleayo yenye makazi hapa Baltimore Maryland. Hii itatoa huduma za upasuaji na uokozi kwa wahanga wa tetemeko hilo. Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Chicago Sun-Times, "It has 250 hospital beds, but can accommodate up to 1,000. The ship's 550-person medical team includes trauma surgeons, orthopedic surgeons, head and neck surgeons, eye surgeons and obstetricians and gynecologists."
Na meli ya tatu ni USS BATAAN
Image from British Sky Tours.com
Imeondoka fukwe za Nolfork kuelekea Haiti kwa shughuli za uokozi. Kwa mujibu wa mtandao wa WVEC.COM, "The amphibious assault ship has a 600-bed hospital aboard, equipped with several operating rooms.
It's also packed full of supplies to help those suffering in the devastated country. Three LCAC hovercrafts will help transport people and goods ashore."

Kila la kheri kwa waokozi wote huko Haiti.

No comments: