Monday, January 18, 2010

"Niko kwenye hali nzuri kwa pambano" Rogers

Bondia Rogers "The Tiger" Mtagwa (pichani juu) amesema yuko kwenye hali nzuri kiafya na kiakili kwa ajili ya pambano lake la kuwania mkanda wa dunia litakalofanyika jumamosi ijayo dhidi ya Yuriokis Gamboa wa Cuba.
Akizungumza nami toka nyumbani kwake Philadelphia katika jimbo la Pensylvania, Rogers ambaye kwa miaka miwili mfululizo amepigana katika mapambano yaliyosemwa na baadhi kuwa "mapambano ya mwaka" (dhidi ya Thomas Villa mwaka 2008 na dhidi ya Juan Lopez mwaka jana) amesema anaendelea vema na mazoezi yake anayofanya mara tatu kwa siku na kuna tofauti kubwa kimaendeleo ukilinganisha na alivyokuwa katika pambano lililopita.
"Najua mpinzani wangu wa sasa ni mzuri kuliko niliyepambana naye awali lakini nami niko kwenye shape nzuri kuliko nilivyokuwa katika pambano la Lopez" alisema Rogers alipozungumza nami.
Pambano hili laonekana kuwa muhimu na gumu zaidi kwa mabondia wote. Rogers ana mapambano mengi zaidi ya kulipwa (professional) japo Gamboa ameshiriki mengi ya ridhaa (amateur)
Nilipomuuliza Rogers juu ya maandalizi na namna anavyoangalia mikanda ya mapambano ya Yuriokis, amesema ameiangalia mikanda yake lakini anajitahidi kuwa katika hali nzuri kimchezo na kutotumia mikanda hiyo kama kigezo pekee cha kumsoma mpinzani wake kwani kama yeye alivyobadilika tangu pambano lake la mwisho mwaka jana, anajua kuna uwezekano Gamboa naye akawa na mabadiliko. Lililo kuu ni kuwa katika hali nzuri na pumzi ya kutosha na kupambana mpaka dk ya mwisho.
Mahojiano ya Mtagwa na Kaka Sunday Simba Shomari yatarushwa usiku wa leo katika matangazo ya SAUTI YA AMERICA idhaa ya Kiswahili. Usikose. Na mahojiano yake na blogu ya Changamoto yetu yatawajia punde nikipata mtunzaji wa sauti online kwani niliyekuwa namtumia (imeem.com) "alitukimbia" bila taarifa.
Tazama Press Conference ya pambano la Jumamosi hapa chini
KILA LA KHERI KAKA MTAGWA.

1 comment:

Anonymous said...

Safi kabisa Mubelwa. Nimependa sana ulivyofanya mahojiano na Rogers. Mimi tangu nimeona clip yake kwenye YouTube mwaka jana nilifurahishwa sana na juhudi zake na ninamwombea mafanikio katika aliloamua kufanya.
Ama kuhusu sauti, soma inbox yako. Shukran sana!
ni mimi unayependa kunipachika jina la ze fundi ze mitambozzzz kidogo kidogo.