Monday, January 18, 2010

POLE DADA CHEMI.


Hayati Rev Douglas G Whitlow (1951 - 2010). Picha kwa hisani Blogu ya Da Chemi
Nimesikitishwa na habari nilizozisoma punde toka kwenye blogu ya Da Chemi kuhusu kifo cha mumewe mpenzi Rev Douglas G Whitlow aliyefariki leo asubuhi. Japo hakuna mengi yanayoweza kumueleza mtu lakini kwa niaba ya familia yangu na FAMILIA NZIMA ya blogu hii twapenda kuungana nwe Dadetu kwenye wakati huu mgumu. Tunataraji kusikia mipango ya mazishi na lolote litakaloendelea.
Twajua amemaliza hatua ya kwanza na ameelekea tuelekeako sote. Na kwa imani twajua tutaishi tena
Tutende mema aliyotenda ili tuje kuwa naye kwa mara nyingine
Msikilize Beres Hammond akisema I'LL LIVE AGAINPOLE SANA KWA DADA CHEMI NA FAMILIA NZIMA

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Poleni sana kwa msiba familia yato ya dada Chemi. Marehemu apumzike kwa amani Amina.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

nami naungana na wadau kumtakia Da Chemi pole. Mnyazi Mungu amjalie utulivu na amani katika kipindi hiki kigumu

malkiory said...

Pole dada kwa msiba. Yote ni mapenzi ya mungu.

John Mwaipopo said...

msiba wetu sote wanablogu. mungu awape subira familia ya chemi che mponda, awajaalie nguvu na kusahau.

Simon Kitururu said...

R.I.P!