Wednesday, January 20, 2010

Jiweke kwenye nafasi zao

Image from NEDARC
Maisha yangu yalibadilika tangu nilipoanza kujiweka kwenye nafasi za watu mbalimbali kabla sijaangalia "makosa" yao. Nimejiweka kwao katika yale waliyonitendea na kuangalia kama ningekuwa mimi niwatendeaye katika kile ninachoamini kulipiza nilichowatendea, je ningejisikiaje? Furaha kwamba nimeipiza kisasi ama? Lakini pia nimekuwa nikijiweka kwenye nafasi zao kujua wanajisikiaje kabla hawajalipiza kisasi kwangu kwa yale wanayoamini nimewatendea? HILI LIMENISAIDIA SAANA KUJUA NAMNA YA KUKABILIANA NA WATU MBALIMBALI.
Na imenifanya nisiwe mgomvi kwani yule anifanyiaye ubaya ili nikasirike, naishia kutabasamu na hilo humfanya aondoke akiwa amejiona ameshindwa kutimiza lengo lake, japo yawezekana kuwa kafanikiwa kunihuzunisha kwa atendalo. Lakini kutoendeleza maasi, nakatisha hivyo. Lakini pia imenifanya kuwafikiria wengine wanavyoumia katika yale ninayowaza kufanya na kuniepusha na kuyatenda. JAMBO ZURI KWANGU PIA.
Lakini sasa kuna wakati ambao mimi na wewe si mtendaji wala mtendewa katika mambo fulani lakini bado twaweza kujiweka kwenye nafasi za watenda na watendewa.
Moja kati ya matukio ni hili la HAITI. Najiuliza kuhusu malaki ya watu waliokufa na wanaoendelea kuharibika barabarani kiasi cha kuzuia usambazaji wa misaada na matokeo yake ni kuwa miili iliyoanza kuharibika imeanza kushindwa hata kutambuliwa na hakuna nguvu kazi za kuanza kuitambua na kuizika ama inavyostahili.
Nawaza miili ya watu ambao familia nzima imefariki na hakuna wa kuitambua, izikweje na nani?
Juzi nilikuwa namuangalia ANDERSON COOPER (One of the greatest and best reporters alive)kwenye kipindi chake cha AC360 na alionesha video hii ambayo alisema INASIKITISHA NA INATISHA LAKINI NI KUONESHA HALI HALISI YA YALIYOWALAZIMU WATU KUFANYA.
MAZIKO YASIYO YA KI-UTU LAKINI UKIJIWEKA KWENYE NAFASI YA WATENDAYO, UNAISHIA KUJIULIZA HATA KAMA HUTAKI KUTOA MALAKI YA MAITI BARABARANI ILI KUWAOKOA WENGINE UNGEFANYA NINI?
Video yake iko hapo chini lakini
ONYO: USIANGALIE KAMA HUWEZI VUMILIA MATUKIO YA KUSIKITISHA.
WARNING: YOU MAY FIND IT VERY, VERY DISTURBING

BLESSINGS

3 comments:

EDNA said...

Inasikitisha sana kwa kweli....Inanifanya niwaze mbali sana enzi za utumwa nakujiuliza huenda bila utumwa wasingepatwa na hili janga, kwa maana wangekuwa somewhere in Africa.Anyway let`s not put blame on anybody yameshatokea,TUMUACHIE MUNGU.

Yasinta Ngonyani said...

Da Edna hata tusikitike vipi hakuna kinachobadilika ni kweli afadhali kama ulivyosema "TUMWACHIE MUNGU"

chib said...

Wazushi wanadai Marekani ndio chanzo cha tetemeko hilo.

Pitia kwenye blogu yangu uchanganyikiwe