Wednesday, January 13, 2010

Msaada kwa wenzetu wa Haiti

May the comfort of God help you during this difficult time.
Ikulu ya Haiti kabla na baada ya tetemeko.
Labda hatuoni na kuumizwa na yanayotokea kwao kwa kuwa HATUKO NAO.
Labda hatuhisi uchungu wa kinachotokea kwa kuwa HATUJAPOTEZA MTU
Labda hatuoni kuwa twaweza kusaidia kwa kuwa TWADHARAU NGUVU ZILIZOMO NDANI MWETU
Labda tunajisahaulisha kuwa ni wenzetu kwakuwa HATUWAFAHAMU
Labda tunaona ni namba ndogo kwa kuwa TWAWACHUKULIA KAMA TAKWIMU
Lakini ndugu zangu na wasomaji wa blogu hii, tuna tunaloweza kuwasaidia ndugu hawa.
HATA MAOMBI TU YANATOSHA KUWASAIDIA
Hali ya Haiti ni mbaya saaana na kwa hakika kila mwenye kuweza kusaidia na afanye hivyo. Najua kila mmoja ana matatizo yake, na mimi nina ya kwangu. Lakini TUKIWAWEKA KATIKA SALA ZETU TUTAKUWA TUMEWASAIDIA SAAAANA.
Hakuna msaada wa mbali na usio na gharama lakini wenye nguvu kama maombi
NAOMBA TUWAOMBEE WATU WA HAITI
Nchi ambayo imekuwa kwenye misukosuko ya vita na uchumi na sasa ilianza kuonesha nia ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake lakini imekumbwa na haya
Nalia ninapoona picha za watoto ambao hata hawajui tafsiri ya TETEMEKO LA ARDHI na wengi wao wamekufa na wengine kupoteza wazazi.
Ni ombi na naamini kila mwenye kumhesabu binadamu kama binadamu na si namba atajua kuwa watu zaidi ya 500,000 wanaohofiwa kufa ni idadi kuuubwa saaaana.
TUWAOMBEE WATU WA HAITI

To all My Brothers and Sisters in HAITI.
Although no words can really help to ease the loss you bear, just know that YOU ARE VERY CLOSE IN OUR EVERY THOUGHTS AND PRAYERS

No comments: