Wednesday, January 13, 2010

Tanzania Yangu.......Izimayo moto kwa petroli

Sentensi ya "kuzima moto kwa petroli" huwa inazungumzia wale ambao wanajitahidi kueleza kuwa wanajali ilhali matendo watendayo ni kinyume na wasemayo. NA HII NDIO TANZANIA YANGU ambayo kila kukicha tunapata ahadi mbalimbali za kuiboresha nchi lakini kila kukicha twaona matendo ya kuibomoa nchi. Tunasikia VITA DHIDI YA RUSHWA , UBADHIRIFU NA UFISADI ambavyo vinaendeshwa na aksari wetu wa Polisi. Lakini tazama makazi yao ukilinganisha na yale ya mafisadi wawalindao. Makazi ya Askari kituo cha Msimbazi Dar Es Salaam Ni vipi unaweza kumwambia mtu kuwa rushwa ni adui wa haki ilhali anaona "analinda mbingu huku akiishi ahera?" Na hawaoni hao wala rushwa , mafisadi / wahujumu uchumi wakiwajibishwa kwa namna yoyote ile. Kitakachofuata ni nini? Akatae rushwa? Tunasikia Rais akizungumza kuhusu kuiboresha ELIMU. NI JAMBO JEMA. Lakini ni vipi unaboresha elimu ilhali watu wanaofanya kazi ya kuielimisha jamii kwa utiifu tena kwa miongo kadhaa wanalazimika "kupiga kambi" zaidi ya mwaka kufuatilia mafao yao? Tena wanatoka waishiko huko mikoani kuja Dar (ambako gharama za maisha ni aghali) na kila siku ni kukimbizana na mafaili yasiyoonekana. HIVI WIZARA YA ELIMU NI KUBWA KIASI GANI KWA MAFAILI KUCHUKUA MWAKA KUPATIKANA? Na hizo kompyuta zinazosemwa kutaka kusambazwa mashuleni kwanini zisianzie wizarani? Ni kweli kuwa wahusika hawajui nani na nani anastahili kustaafu lini? Kama hawajui, basi ina maana kuna waliofikisha umri wa kustaafu na wanaendelea kulipwa na kama wanajua basi wanatenda uzembe makusudi ili watu wachoke kufuatilia pesa hizo na wao wazikamate "kwa niaba yao". NI UJINGA NA UONEVU Tarehe 23 mwezi huu, Rogers Mtagwa anapanda ulingoni kugombea mkanda wa Dunia wa WBA. Ni kwa juhudi zake na si msaada wa serikali INYOHIMIZA MICHEZO Hasheem kafika alikofika kwa juhudi zake na si serikali INAYOHIMIZA MICHEZO. Lakini uliona mapokezi yake? Jikumbushe hapa Picha kwa hisani ya Mtandao wa Bongo Celebrity
Nimemsikia Waziri na Rais wakipongeza wachezaji wetu wanapofanya vema lakini wanashindwa kujua kuwa wanahitaji kuwekeza kwenye michezo na elimu kwa pamoja. Yaani wanachofanya Rais na Waziri kuzuia michezo ni kusema HAKUNA MUSTAKABALI (FUTURE) WA MICHEZO NCHINI AMA KAMA UPO, BASI TUWE NA WACHEZAJI WASIOKWENDA SHULE kwani ili ushiriki michezo basi usiende shule ama uende shule na ukose michezo. Hawaoni wenzao wanasomesha watu lwa scholarship za michezo na hata kina Hashm Thabiti wamepata nafasi ya kutumia vipaji vyao vya michezo kusoma. AIBU KWAO.
Magomeni iliyoachwa na mkoloni. Ilikuwa inaeleweka mitaa na mipango miji. Nenda sasa uone. Picha kwa hisani ya Michuzi Blog Najua wananchi wanahadaishwa kuwa maendeleo ni hivyo "vikwangua anga" lakini najiuliza tunakoelekea bila maegesho na barabara za kutosha. Bila mifumo ya majitaka. Hivi hawa wote waki-flush vyoo na mtaro ukaziba Dar si itafurika kwa maji-choo? Picha toka PBase.com 
Nasikia mikataba inasainiwa ya kuendeleza mji (hasa Dr) na "vikwangua ana" vinazidi kuongezeka, lakini kinachosikitisha ni kuwa DAR ES SALAAM YA MKOLONI ILIKUWA IMEPANGWA NA KUJENGWA VEMA KULIKO AMBAVYO INAWEZA KUWA MWAKA 2015 Na majengo "yanayoota" bila kuona ukarabati na upanuzi wa mifumo ya maji, umeme na majitaka na hata maegesho na barabara. Kwa nje yaonekana kama maendeleo lakini nahisi tunakaliza "bomu la vinyesi" kwani mitaro ikiziba sijui hao wawekeza tunaowaalika tutawatoaje kwenye mafuriko ya majitaka? Lakini hii ndiyo TANZANIA YANGU. Ihimizayo "elimu ya ukarabati, ivunayo isipopanda, iuzayo baiskeli kununua kengele, irembayo ghorofa ikipuuza msingi, iliyo bize kumwagilia matawi badala ya mizizi na yenye kuzima moto kwa petroli.
Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"

5 comments:

Born 2 Suffer said...

Tanzania ni nchi nzuri sana katika nchi za africa cha kushangaza usafi katika jiji unawashinda vipi? Jiji la dar likwa safi litapendeza sana watanzania fanyeni jiji liwe safi, Bora kuweka sheria eneo lolote karibu ya duka au soko lipo chafu wapigwe faini wahusika wa sehemu hio, na mpita njia yeyote yule akionekana kutupa uchafu njiani kukamatwa na kupigwa faini labda itasaidia na hivi ndivyo nchi nyingi za ulaya zinafanya haswa Singapore ndio maana miji yao inakua daima misafi.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

hiyo ndo bongo-daslam kaka :-(

Godwin Habib Meghji said...

TaTHIMINI NZURI, ITAWEZEKANA TU PALE KIZAZI HICHI KITAACHA UBINAFSI.

Anonymous said...

Yani we kaka unanibariki sana na mada zako unazokuja nazo kwenye blog yako,inaonyesha tu jinsi ulivyo na matumizi mazuri ya ufahamu.
Mungu akubariki

Mzee wa Changamoto said...

Asanteni saana WANDUGU kwa kuendeleza mapambano.
Asante na Baraka kwako Anonymous.Kwa bahati mbaya sina mawasiliano yako ninayoweza kuyatunza na ya wapendwa wengine.
HESHIMA KWENU NYOTE