Tuesday, January 12, 2010

Aibu kwa tasnia ya habari Tanzania

Februari 4 mwaka jana niliandika bandiko nililolipa kichwa cha habari Dah!!! Waandishi wetu jamani (bofya hapa kuirejea) nikisikitishwa na uandishi wa wanahabari wetu Tanzania ambao kwa hakika WANACHEFUA. Na ninapenda kurejea nilichoandika kwani bado kingali sahihi na nilisema "Waandishi wa nyumbani wengi wao ni wavivu wa fikra na hawatafuti ukweli wa kile wanachoripoti."
Ndio ukweli unaoendelea kujidhihirisha kila kukicha nyumbani na tukio lililotokea hivi karibuni linasikitisha zaidi na linanigusa mimi na WANACHANGAMOTO WOTE kwa kuwa tumekuwa chanzo cha hilo lililotokea. Jumamosi ya Jan 9 niliweka bandiko kwenye mtandao wa WANABIDII lenye kichwa cha habari NIONAVYO MIMI... UCHAGUZI WA RAIS
NA WABUNGE UTENGANISHWE (Bofya hapa kuisoma kwa usahihi)
ambalo pia nilitangulia kulibandika hapa Julai 14 mwaka jana. Lakini licha ya kuliweka bandiko hilo kwa nia njema na kusaka uchambuzi na utambuzi wa kina kuhusu umuhimu na uwezekano wa hoja niliyoiweka, mwandishi MOBINI SARYA wa gazeti la TANZANIA DAIMA ameamua kuandika kilicho tofauti kabisa na aliyoshauri Kaka Zitto na kusababisha mgongano wa mawazo kwa waTanzania wengi. Mwandishi Sarya ameamua kutumia baadhi ya nukuu toka katika mchango wa Kaka Zitto na kuzibadili kumfanya aonekane anataka Rais Kikwete aongezewe muda jambo ambalo SI SAHIHI. Naomba nyote msome MCHANGO WA KAKA ZITTO KABWE HAPA na kisha linganisha na ANDIKO LA TANZANIA DAIMA HAPA kuona ambavyo waandishi wanapindisha maandishi kwa manufaa yao.
Nilishaandika HAPA kuhusu VYOMBO VYA HABARI TANZANIA VISIVYO NA HABARI ZAIDI YA TAARIFA na nilishaandika kuhusu UVIVU wa waandishi ambao wanategemea kila kitu kutoka kwa wengine na tunaona ambavyo tatizo hili linakua. Mwandishi hakumsaka Mhe. Zitto kumuuliza kama alimaanisha kuongezwa muda kwa Rais Kikwete na wala hakutaka kupata maoni ya wanasayansi wa siasa na hakuwa na hakika kama kilichoandikwa ni maoni ama maamuzi (ambayo Mhe. Zitto hana uwezo wa kuyatoa)
Kwa ufupi, mwandishi HAKUJUA CHA KUANDIKA NA ALILAZIMISHA KUWA "ACTIVE" KWA KUONEKANA NAYE ANA STORY AMBAYO "KAIIBA" MTANDAONI NA KAIKOSEA.
Hii ni AIBU KWA TASNIA YA HABARI TANZANIA


2 comments:

Anonymous said...

Ni wakati wa uchaguzi huu na huwezi jua who is who. Zito mwenyewe I believe ni CCM - Mrema type na hizi habari may be true. Ya hawa wanasiasa hayaeleweki especially now that we are going to election. RUSHWA TUSHWA tu

Godwin Habib Meghji said...

Nasikitika kusema hili. WAANDISHI WENGI WA TANZANIA(SI WOTE) NI WAVIVU WA KUTAFUTA HABARI NA NI WAVIVU ZAIDI WA KUCHAMBUA HIZO HABARI. Kutokana na uvivu huo, ndio maana inakuwa rahisi sana kwa muandishi wa habari kurubuniwa na kutumiwa. Habari nyingi wanaandika si kwa kufuta taaluma zao, bali kumridhisha mtu fulani. SIKUJUA KWAMBA BONGO KAMA UNA TUKIO NA UNATAKA LIWE KAVADI NA MEDIA LAZIMA UWALIPE WAANDISHI WA HABARI WANAOKUJA. Nilishtuka zaidi pale klabu ya usiku ya maisha ilipoungua. Yule mama baada ya kuongea na waandishi wa habari mwisho wa siku ilibidi atoe bahasha kwa watu hawa wasio na aibu kuwa mtu huyu yupo kwenye matatizo. KAMA MTU ANAWEZA KUFANYA HIVI, SISHANGAI KAMA ATASHINDWA HATA KU KOPI NA KUPESTI TAARIFA AMBAZO HAZINA UKWELI WA AINA YEYOTE