Friday, January 8, 2010

Them, I & Them.....WHEN......Nasio Fontaine

Picha toka COZAY.COM
"Nimekaa dirishani nikiiwaza kesho kisha najiuliza mustakabali utakavyokuwa.
Nawafikiria watoto walio wahanga wa ukandamizaji.
Wanaojeruhiwa na vita na kukondeshwa kwa njaa
Ni lini VITA HII MBOVU itaisha na watoto kupata fursa ya kwenda nje kucheza?
NATAKA KUONA
Siku ambayo ukandamizaji utakoma na watu kushangilia wakisema HATIMAYE UHURU UMEWASILI."

Haya si maneno yangu bali ni tafsiri isiyo rasmi ya wimbo WHEN wake NASIO FONTAINE alioimba akiuliza na kueleza raha na faida ya siku tutakapoona amani ya kweli duniani.
Nasio ameimba saana kuhusu AMANI YA KWELI na ameisema kwa undani wake katika nyimbo zake nyingine. Amewazungumzia ma-babylon wanaozungumzia amani hadharani huku wakiwa vyanzo vya vita katika vikao vyao vya siri. Lakini Nasio ameendelea kulilia amani ya kweli kutoka kwa wale wafanyao maamuzi na kutoka kwa wawachaguao, na kuendelea kuonya kuwa VITA SI SULUHISHO na halitatokea kuwa suluhisho. Alisema haya katika wimbo wake wa Babylon "war is not the solution. Never was, never will it be so". Na bado anaonya kuhusu kuutazama ulimwengu kwa JICHO LA NDANI kwani walio katika MEDITATION wanaona vita vinavyofukuta huko vilipo anaposema "And I can hear the voice of the sufferers cry for justice. Uhh, another ugly war is a raging, threats of nuclear war is arising and the world is gripped by fear of mass destruction" Na huu ndio ukweli ambapo dunia inakimbizana na isyowajua kutaka kuhakikisha hawana silaha za maangamizi ambazo wao wanaruhusu kuendelea kuwepo.
Inasikitisha.
Msikilize ukifuatilia maandishi hapa chini


Oh nah nah nah nan nap
Oh na na na nam nam
Oh na na, nam nam ohh, uhh
Yeeaahh, yyeeaahh, ohh ohhu ohhwu,

Looking out my window
And I’m a thinking of tomorrow
And I’m a wondering what the future will be
Thinking of the children
Who are the victims of oppression
Beaten down by wars, and eaten up by starvation

And I’m saying
When will this ugly war be over
And the children can go out and play
I wanna see
When will all oppression will be done
And the people will rise up and say

Freedom at last, freedom at last, so free
Freedom has come, freedom has come, ohh yeahy

See I, sitting in seclusion
And I’m in my meditation
And I can hear the voice of the sufferers cry for justice
Uhh, another ugly war is a raging
Threats of nuclear war is arising
And the world is gripped by fear of mass destruction

I’m a saying
When will this ugly war be over
And the children can go out and play, I wanna see
When will all oppression will be done
And the people will rise up and say

Freedom at last, freedom at last, so free,
Freedom has come, freedom has come,
Oh yeahy, oh uh yeah, nuh

Umhm mm, so much bloodshed and sorrows
There is no future for the youths of tomorrow, yeah
So many mothers crying
Too many funerals, oohh
When will it end

Saying, when will this ugly war be over
And the children can go out and play, I wanna see
When will all oppression will be done and the people will rise up and say
Freedom must come uuh, uhh, mhn



**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Maria said...

Asante kwa ujumbe wenye nguvu!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Askante, lakini kwa nini UIWAZIE KESHO? Inakuhusu nini ilhali haijafika? :-(